Monday, 13 October 2014

KUTANA NA KIJANA ANAYEKUNYWA DAMU KABLA YA KUFANYA KAZI
















Untitled
Kijana wa miaka kumi na 19 anayeitwa Jamal Nasiru kutoka Nigeria
amekamatwa na chombo cha dola kinachohusika na kudhibiti ukabaji (SARS)
baada ya kukiri kunywa damu ya ng’ombe kabla ya kufanya kazi yake ya
uporaji na ukabaji.

Kijana
huyu alikiri kutumia damu hiyo kumsaidia kumlinda yeye na kundi lake
kila wakitaka kufanya kazi zao za uporaji, vijana hao walikamatwa baada
ya damu hiyo ya ng’ombe kushindwa kufanya kazi ambapo mkuu wa kundi hilo
alithibitishwa kuuwa kwenye mapigano kati ya kundi la waporaji hao na
askari.
Baada
ya kijana huyu kuhojiwa alisema ‘ Nashangaa sikuweza kutoroka siku
ambayo nilikamatwa na siwezi kukumbuka nimeua watu wangapi wakati
nafanya kazi, watu ambao niliwaua ni ambao walikataa kutii amri ambazo
nilikuwa nawapa’.
Aliendelea
kusema kuwa sababu ya yeye kujiingiza kwenye biashara hizo za ukabaji
ilitokana na kulipwa pesa ndogo kutoka kwenye kazi yake ya ulinzi, baada
ya muda mfupi aliona kuwa kazi hiyo inampotezea muda kwahiyo akaamua
atafute njia nyingine ya kumpa pesa ndio akamtafuta rafiki yake mwenye
jina laitwae Umaru Akubaka aliyemtambulisha kwenye kundi hilo la uporaji
na ukabaji.
Mtuhumiwa
alisema yeye na kundi lake walifanya shughuli zao kwenye mji wa Lagos
ambapo walikamatwa baada ya kumuua mlinzi tarehe 11 Mei mwaka huu na
akakiri kuwa walipewa silaha na mkuu wa ulinzi wa Omole Estate na
kuzitumia kukaba wasafiri wa njia za miguu au kuny’anganya magari kwenye
njia panda au gari ambazo zimewekwa kwenye ukingo wa barabara.
Polisi wametoa ripoti na kusema mtuhumiwa huyu atapewa adhabu yake baada ya uchunguzi kumalizika.
via>>Babamzazi.com

No comments:

Post a Comment