Jeshi la Polisi mkoani Arusha limefanikiwa kumuua jambazi aliyekuwa anajihusisha na mauaji ya wanawake mkoani humo ajulikanae kwa jina la Ramadhani Abdallah Jumanne mwenye umri wa miaka 37.
Jamabazi
huyo ambaye alikuwa anasakwa kwa muda mrefu aliuawa katika majibizano ya risasi
yaliyotokea usiku wa wa kuamkia leo wakati ambao Polisi walifika anapoishi
jambazi huyo kwa ajili ya kumkamata.
Taarifa zilizothibitishwa na kamanda mkuu
wa Polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas zinaarifu kuwa, Jambazi huyo ametambuliwa na baadhi ya wanawake na alikufa
muda mchache alipokuwa anakimbizwa hospitali ya mkoa wa Arusha kwa ajili ya
matibabu ili badae afanyiwe upelelezi.
Kabla
ya kifo chake Jambazi huyo alikuwa akifanya mauaji hayo kwa kutumia pikipiki
ambapo yeye na mwezake ambaye ni dereva walikuwa wanawaua wanawake watembea kwa
miguu na baada ya hapo wanachukua baadhi ya viungo kwenye miili ya wanawake hao
na kukimbia.
Polisi
walimkuta jambazi huyo na risasi pamoja na bastola aina ya SMG na maiti yake
iko Makao makuu ya Polisi Arusha.

No comments:
Post a Comment