
Familia ya Baba wa Taifa, Hayati mwalimu
Julius Kambarage Nyerere imeuomba uongozi wa Benki Kuu ya Tanzania
kuiondoa katika mzunguko wa fedha noti ya shilingi elfu Moja yenye picha
ya Baba wa Taifa kwa maelezo kuwa picha hiyo si sahihi.
Madaraka Nyerere, Msemaji wa familia ya Mwl Nyerere
Familia ya baba wa taifa hayati mwalimu
Julius Kambarage Nyerere imeuomba uongozi wa Benki Kuu ya Tanzania
kuiondoa katika mzunguko wa fedha noti ya shilingi elfu Moja yenye picha
ya Baba wa Taifa kwa maelezo kuwa picha ambayo imetumika katika noti
hiyo haifanani kabisa na kiongozi huyo na kwamba kuendelea kutumika ni
sawa na kumdhalilisha muasisi huyo wa taifa la Tanzania.
Akizungumza kwa niaba ya familia na ukoo
wa Baba wa Taifa wakati wa kupokea mradi wa kuboresha makumbusho ya
Mwalimu Nyerere na kuzindua onesho la noti na sarafu ambazo zimetumika
katika vipindi tofauti kuanzia mwaka 1967 hadi sasa zenye picha na
sahihi ya Baba wa taifa, mmoja wa watoto wa Baba wa taifa Bw Madaraka
Nyerere, amesema picha iliyopo katika noti hiyo ya shilingi elfu Moja
haifanani na sura ya kiongozi huyo hivyo kuomba benki hiyo kuangalia
uwezekano wa kuiondoka katika mzunguko.
Naye Kaimu Gavana wa benki kuu ya
Tanzania Bw Juma Reli, pamoja na kutoa ahadi ya ukarabati nyumba ya
kwanza ya Baba wa Taifa ambayo aliitumia kabla ya kujengewa na TANU
amesema kuwa benki hiyo imejitolea kuboresha makumbusho hayo ili
kuhifadhia kumbukumbu zenye histori ya baba wa taifa kwa ajili ya vizazi
vya sasa na vijavyo.
Kwa upande wao mkurugenzi mkuu wa
shirika la makumbusho ya taifa Profesa Audax Mabula na mkuu wa wilaya ya
Butiama Bi Angelina Mabula, wameishukuru benki kuu ya Tanzania kwa
kutambua umuhimu wa kuboresha makumbusho hayo katika kuhifadhi
kumbukumbu mbalimbali za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ili
kulinda historia za kiongozi huyo.
No comments:
Post a Comment