Naodha wa kikosi cha timu ya Benini Stephane Sessegnon amesema amesema anaamini mchezo wa kesho wa kirafiki
na timu ya taifa ya Tanzania utakuwa mgumu,lakini amesisitiza kuwa lingo la ni kushinda katika mchezo huo utakaopigwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
na timu ya taifa ya Tanzania utakuwa mgumu,lakini amesisitiza kuwa lingo la ni kushinda katika mchezo huo utakaopigwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
| Stephane Sessegnon akiwa katika klabu yake ya sasa West Bromwich Albion |
| Stephane Sessegnon akiwa Paris Saint-Germain ya Ufaransa |
| Stephane Sessegnon akiwa Sunderland ya England |
Akizungumza na waanisshi wa habari mapema hii leo Stephane Sessegnon mchezaji wa West Bromwich Albion ambaye amechezea vilabu kadhaa vya ulaya kama Paris Saint-Germain ya Ufaransa na Sunderland ya England amesema haifahamu vizuri Timu ya Tanzania lakini lengo lao ni kushinda.
Akizungumzia swala la linalosemekana kuwa wachezaji wa Afrika wanaocheza ulaya huwa hawajitumi katika timu zao za Taifa,Sessegnon amekiri
kuwa tatizo hilo lipo kwa wachezaji wengi wanapokuja Afrika kwa sababu
klabu wanazochezea huwa wanawapa masharti kwa kuhofia kuumia,lakini Sessegnon amesema yeye ni mpiganaji na kuahidi kesho atafanya vizuri katika timu yake ya Benini.
Akijibu
swali la mwandishi wa habari za michezo,Mchezaji huyo wa West Bromwich
Albion pia amezungumzia swala la wachezaji wengi wa Afrika kutopewa
nafasi kama kutambuliwa na kupewa tuzo wanapofanya vizuri katika timu za
ulaya,akisema hiyo ni hali ya kawaida hata yeye imemtokea akiwa
Ufaransa na kusisitiza yeye hajali hilo kwani anachoangalia ni kufanya
kazi.
Kikosi
cha wachezaji 18 na viongozi 11 wa timu ya Taifa ya Benin, kimetua
jijini Dar es Salaam tayari kwa mechi ya Kalenda ya FIFA dhidi ya Taifa
Stars itakayochezwa Jumapili (Oktoba 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Wachezaji
wa timu ya Benin ambayo imefikia hoteli ya JB Belmont waliwasili Juzi
(Oktoba 9 mwaka huu) Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNIA) kwa nyakati tofauti.
Kikosi
hicho kitafanya mazoezi yake ya kwanza jana (Oktoba 10 mwaka huu) saa
10 jioni kwenye Uwanja wa Gymkhana. Benin watafanya mazoezi yao ya
mwisho leo (Oktoba 11 mwaka huu) saa 10 jioni Uwanja wa Taifa.
Wachezaji
walioko kwenye kikosi cha Benin ni Stephane Sessegnon (West Bromwich
Albion, Uingereza), Didier Sossa (USS Krake, Benin), Abdel Fadel Suanon
(Etoile Sportive du Sahel, Tunisia), Jodel Dossou (Red Bull Salzburg,
Austria), Sessi D’almeida (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa), Mohamed
Aoudou (JS Saoura, Algeria) na Saturnin Allagbe (Niort, Ufaransa).
Steve
Mounie (Montpellier, Ufaransa), Farnolle Fabien (Clermont Foot Auvergne
63, Ufaransa), Jordan Adeoti (Caen, Ufaransa), Michael Pote (Omonia
Nikosia, Cyprus), David Djigla (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa) na
Seidou Baraze (Kawkab Marrakech, Morocco).
Jean
Ogouchi, Centre Mberie Sportif Club, Gabon), Nafiou Badarou (ASO Chlef,
Algeria), Eric Tossavi (Avrankou Omnisport, Benin), Fortune Ore (USS
Krake, Benin) na Seibou Mama (Aspac, Benin).

No comments:
Post a Comment