Sehemu ya ukumbi ulioharibiwa vibaya na washabiki mjini Stuttgart, Ujerumani.
Usiku wa Jumamosi Agosti 30, 2014, majira ya saa 10 alfajiri, mwanamuziki nyota wa Bongo Flavor, Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz alijikuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart, Ujerumani, baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show.
Mashabiki hao waliokuwa wamelipa tiketi
euro 25 kwa kiingilio walihadiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku,
lakini walijukuta wakisubiri hadi majira ya saa 10 alfajiri ndipo
mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria
anayejiita Britts Event.
Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa
hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki
Diamond na promota wake, Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na
vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya
mashabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki, ma-Djs walishambuliwa na wapo
hospitalini kwa sasa.
Mmoja wa Djs hao alipoteza lap top yake,
mwanadada DJ Flor alipatwa mstuko wa moyo na kukimbizwa hospitali,
washabiki hao walimpa kipigo DJ Drazee naye yupo hoi hospitali. Polisi
nchini Ujerumani wanamesema tukio hili la aibu halijawahi kutokea, kuwa
msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa Ujerumani ni kitu cha hatari kwani
washabiki wa Ujerumani wanaheshimu sana muda wao.
Mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa
onyesho hilo na wamesema wanachunguza thamani ya hasara iliyosababishwa
na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promota huyo raia wa
Nigeria ambaye pia anachunguzwa kwa kujihusisha na mtandao fulani wa
biashara.
No comments:
Post a Comment