Jeshi
la polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga Jana lililazimika kutumia
risasi za moto baada ya wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa kuua
watuhumiwa kisha kuwachoma moto.
Inasemekana
watuhumiwa hao walivamia chumba ya mkazi mmoja wa mtaa wa Muhungula
Kahama na kujeruhi kwa mapanga watoto wawili usiku wa kuamkia jana.
Kwa
mujibu wa habari kutoka wilayani Kahama, juzi usiku watu 7 wanaodaiwa
kuwa ni vibaka walivamia nyumba ya mtu kisha kujeruhi watoto wawili.

Kufuatia tukio hilo wananchi walianza kufanya msako kubaini watuhumiwa hao ,ndipo wakakamata wawili kati yao na kuanza kuwachoma moto.

Kufuatia tukio hilo wananchi walianza kufanya msako kubaini watuhumiwa hao ,ndipo wakakamata wawili kati yao na kuanza kuwachoma moto.
Wakati
tayari wananchi wameshaua mmoja,jeshi la polisi lilifika kwa ajili ya
kumwokoa mmoja,lakini wananchi hawakukubaliana na hali hiyo wakaanza
kushambulia kwa mawe gari la polisi ndipo jeshi la polisi likaanza
kufyatua risasi za moto.
Maafisa wa jeshi la Polisi wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wakiwa katika eneo la tukio kwa ajili ya kuuchukua mwili wa Marehemu.
Maafisa wa jeshi la Polisi wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wakiwa katika eneo la tukio kwa ajili ya kuuchukua mwili wa Marehemu.

No comments:
Post a Comment