Staa
wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson amenaswa laivu kimahaba nchini
Marekani akiwa na msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Kassim Mganga.
Wakati mumewe Sunday Demonte akidaiwa
kuwa yuko mbioni kuhukumiwa kwenda jela huko Dubai, staa wa Bongo
Movies, Aunt Ezekiel Grayson amenaswa laivu kimahaba nchini Marekani
akiwa na msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Kassim Mganga.
Wakati anaondoka nchini hivi karibuni,
Aunt alionekana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
jijini Dar, akiwa na mwanaume ambaye anadaiwa kuwa ni mume wa mtu, Moses
Iyobo ‘Moze’.Baada ya habari hiyo kuripotiwa na paparazi mwaka huu,
ilidaiwa kwamba ndugu wa mumewe, Sunday hawakufurahishwa na kitendo
hicho.
“Tunashangaa kumuona Aunt ameambatana na
mume wa mtu na huko anakoenda pia tunasikia watakuwa wawili tu na
Kassim, inatutia shaka kwa kweli,” alisema mmoja wa ndugu wa mume kwa
sharti la kutoanika jina lake.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo
nchini Marekani, wawili hao walitia maguu hivi karibuni kwa mwaliko
maalum wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo ambapo Kassim alipewa nafasi
mbili hivyo akaamua kumchukua Aunt.
“Kassim aliambiwa atafute kampani ya
kuja nayo huku ndipo akaona Aunt anafaa kwa kuwa mwenyewe amedai ni mtu
wake wa karibu,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data
kwamba, baada ya wawili hao kufika nchini humo, walipanga katika hoteli
moja kisha kuanza kujiachia kwenye viwanja tofautitofauti wakila bata
ndani ya Jiji la New York.
Baada ya mwanahabari wetu kunasa mchapo
huo, alimtafuta Aunt kupitia WhatsApp hakupatikana, bahati nzuri Kassim
alipatikana na kusema:“Tumekuja kwa mwaliko wa ubalozi wetu, Aunt ni
mshkaji wangu kwa hiyo usishangae sana nikila naye bata,” alijibu
Kassim.
No comments:
Post a Comment