Wafanyabisahara jijini Mwanza leo wameanza mgomo wa kutofungua maduka yao kwa siku zisizojulikana kwa kile walichodai Mkurugenzi wa jiji hilo, Hassan Hida amekataa kukutana nao kwa lengo la kujadili changamoto zinazowakabili.
Mgomo huo utakuwa wa pili kufanyika baada
ya mara ya kwanza kutokea wakati wafanyabiashara hao wakigomea matumizi ya mashine za
Stakabadhi za Elekitroniki (EFD).
Hata
hivyo mgomo huu ulioanza leo hauhusishi tena mashine za EFD badala yake
umejikita katika matatizo yanayowakabili ambayo ni ongezeko la kodi ya taka
kutoka Sh 8,000 hadi 10,000, kutoza fedha za kuweka bidhaa zao nje ya
duka na mambo mengine ya kukamatiwa mali zao.
Uamuzi huo ulifikiwa
juzi katika mkutano mkuu ulioitishwa na Jumuiya ya Wafanyabiashara
Tanzania (JWT), mkoa wa Mwanza kwa lengo la kutoa taarifa za mazungumzo
kati ya Serikali juu ya matumizi ya mashine za EFD.
Kabla ya kufikia
azimio la kutofungua maduka yao, Mwenyekiti wa JWT, mkoa wa Mwanza,
Christopher Wambura aliwaeleza wafanyabiashara hao jitihada alizofanya
za kukutana na mkurugenzi huyo mara zote ziligonga mwamba.
“Ndugu
zangu wafanyabiashara mliniagiza pamoja na viongozi wenzangu tutafute
suluhisho la matatizo yanayotukabili katika biashara zetu hapa jijini
Mwanza, wakati tunahangaika hapa kwetu, viongozi wa kitaifa wa JWT nao
walikuwa wanahangaika huko Dar es Salaam.
“Kwa bahati nzuri uongozi
wa kitaifa umefanikiwa kwenda Ikulu na kukutana na wawakilishi wa Rais
Jakaya Kikwete, baada ya hapo walikutana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ndio maana leo
mnaona hakuna usumbufu juu ya mashine za EFD.
“Wakati usumbufu wa EFD
ukiwa umepotea, kero zetu zinazotukabili hapa
Mwanza bado hazitaki kutatuliwa na uongozi wa jiji, mkurugenzi
anatukimbia kila tunapopanga kukutana naye.
“Tumefanya jitihada za
kukutana na Mkuu wa Mkoa, Evarist Ndikilo, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana,
Baraka Koni na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Titto Mahinya wote walionyesha
jitihada za kutusaidia kukutana na mkurugenzi lakini hatukukutana mpaka
leo hii,”alisema.
Wambura alisema pamoja na jitihada hizo, mara zote
mkurugenzi amekuwa akiwaeleza kutokuwa na nafasi ya kukutana nao kwa
kile alichodai kubanwa na majukumu ya kazi pamoja na kuwa nje ya mkoa
kwa shughuli maalumu.
Pamoja na masuala mengi yaliyozungumzwa hapo,
wafanyabiashara na viongozi wao walikubaliana kutofungua maduka yao hadi
hapo mkurugenzi atakapokutana nao huku wakisisitiza na kutoa onyo kwa
wale watakaokiuka maazimio yao.
Mkurugenzi anena
Mpekuzi
ilimtafuta Mkurugenzi wa jiji hilo kwa njia ya simu, ambapo alisema
yupo nje ya ofisi, lakini amewataka viongozi wa JWT wakutane naye
kesho saa nne ofisini kwake.
“Nipo
nje ya ofisi, muda huu siwezi kuzungumzia mgomo huo, lakini
nimewaomba wafungue maduka yao halafu Viongozi wao wafike
Ofisini kwangu kesho saa nne tuzungumze,” alisema kwa ufupi.
TRA Mwanza
Kwa
upande wa Meneja wa TRA mkoa wa Mwanza, Jeremia Lusana amesema kitendo
cha wafanyabiashara hao kugoma kinasababisha hasara kubwa katika
suala la mapato huku akitishia kuwafungia lenseni za biashara zao.
“Tumechoka
kutishwa na mgomo wa wafanyabiashara hao, umefika muda wa kuangalia
namna ya kuwafungia leseni zao ili wakae nyumbani, biashara yao ina
manufaa kwao na sisi, kipindi kile tulipata hasara kwa sababu mgomo
ulishtukiza." Amesema Lusana
Lusana
amesema TRA haina uwezo wa kuwalazimisha kufungua maduka, hivyo
watasubiri hadi hapo watakapofungua ndipo watakapoendelea

No comments:
Post a Comment