
BILIONEA William Henry "Bill" Gates naye ameungana na mastaa mbalimbali katika kupambana na ugonjwa wa Amyotrophic Lateral Sclerosis (ALS), maarufu kama Lou Gehrig kupitia kampeni ya ‘Ice Bucket Challenge’.
Video iliyowekwa katika mtandao wa
kijamii wa Facebook na kijana Pete Frates wiki mbili na nusu zilizopita
imewavutia watu wengi wakiwemo Justin Bieber, LeBron James, Chris
Christie and Taylor Swift ambao wamechukua ndoo ya maji baridi kuungana
katika kampeni hiyo.
Ugonjwa wa ALS hushambulia seli za
mishipa ya fahamu na kupelekea mgonjwa kupata matatizo katika kuongea,
kumeza, kupumua na baadaye kupooza. Mpaka sasa watu takribani 30,000
nchini Marekani wana ugonjwa huo.
Kampeni ya ‘Ice Bucket Challenge’
hufanyika kwa watu kutengeneza video zao wakijimwagia ndoo ya maji
baridi kichwani kisha kuzituma katika mitandao ya kijamii na kuwataka
wenzao kufanya hivyo pia ndani ya masaa 24 au kuchangia dola za
Kimalekani 100 kwa Chama cha ALS ambapo mara nyingi watu hufanya vyote
(kujimwagia maji na kuchangia fedha).
No comments:
Post a Comment