Kumekuwa na
msisimko mkubwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii nchini
Kenya kuhusu taarifa ya msichana wa Kihindi aliyekiuka mila na tamaduni
za jamii yake na kuolewa na kijana Mwafrika.
Msichana huyu
wa kihindi anaitwa Sarika Patel, na ameolewa na kijana wa kabila la
Bukusu Timothy Khamala, jambo ambalo ni nadra sana kwa watu wa jamii ya
kihindi. Kilichowashangaza wengi ni kwamba Sarika ametoka katika familia
tajiri na kuamua kuishi maisha ya walalahoi kijijini
Kwa Sarika
maisha ya umaskini ambayo Timothy anaishi sio kikwazo hata kidogo bali
kwake hapo ndipo anapata raha na mapenzi ambayo anasema yamemridhisha na
kumtuliza nyumbani kwa kijana Timothy.
Timothy
alikuwa anafanya kazi nyumbani kwa kina Sarika kama mjakazi lakini
akafutwa kazi na baba ya Sarika baada ya kupendana na msichana wake.Kwa
sasa yeye ni tarishi katika ofisi hii ya jimbo.Sarika hana kazi
Wawili hao
sasa wapo katika pilka pilka za kuanza maisha mapya ila kwa pingamizi
kali . Sarika Patel anasema kulingana na mila yao si sawa kuolewa na mtu
asiyekubaliwa au kuchaguliwa na wawazi wako. Wachumba kwa kawaida
hutoka jamii sawa.
No comments:
Post a Comment