Video Queen wa mwanamuziki Sunday Mangu ‘Linex’ aliyeng’arisha Wimbo wa Ifola, Janeth Bundala amedai kutishiwa maisha na mfanyabiashara mmoja aliyemtaja kwa jina la Johari Ali, kisa kikiwa ni kuzaa na aliyekuwa mpenzi wake.
Akizungumza na paparazi, Janeth alisema
mama huyo ambaye anamheshimu sana hakutarajia kama angeweza kumtishia
maisha wakati mwanaume anayetajwa alishaachana naye.
“Yule mwanaume niliyezaa naye ni kweli
alikuwa mpenzi wa yule mama lakini walishaachana, sasa nashangaa
ananitumia sms za vitisho.
Nimekwenda kutoa taarifa polisi na
kumfungulia jalada la kesi lenye namba KJN\RB\6333/14, chochote
kitakachonikuta ataisaidia polisi,” alisema Janeth.
Paparazi alimpigia simu Johari na kumsomea mashitaka yake ambapo alisema yuko China na hamjui Janeth.
>>BOFYA HAPA<<
Paparazi alimpigia simu Johari na kumsomea mashitaka yake ambapo alisema yuko China na hamjui Janeth.
>>BOFYA HAPA<<
No comments:
Post a Comment