Hospitali
ya Chuo cha Kimataifa cha Matibabu na Teknolojia (IMTU) kinachohusishwa
na utupaji wa viungo vya binadamu mithili ya takataka, imefungiwa kwa
muda usiojulikana baada ya kugundulika kutokidhi viwango na maadili ya
utoaji huduma za hospitali nchini.

Manispaa
ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
imechukua jukumu la kuifungia hospitali hiyo baada ya kufanya ukaguzi wa
kushitukiza na kubaini uwepo wa mapungufu kadhaa.

Mapungufu
yaliyobainika kuwepo katika hospitali hiyo ni pamoja na kutokuwa na
wauguzi wa kutosha, kutokuwa na vifaa vya kutosha ikiwemo kifaa cha
kuchomea taka ngumu, kuchanganya dawa zilizokwisha muda na ambazo
hazijaisha muda wake na pia wauguzi kufanya kazi ambazo si za kwao.

Akizungumza
wakati wa kufunga hospitali hiyo, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni,
Dk Gunini Kamba alisema, hospitali hiyo inastahili kufungiwa kutokana
na kutokidhi viwango hivyo.

"Baada
ya kufanya ukaguzi wa kushitukiza tumebaini kuwepo kwa mapungufu haya,
kwa hiyo tunaifungia hospitali hii mpaka pale watakaporekebisha," alisema Dk Kamba.

Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Profesa Yassin Mgonda
alikiri kuwepo kwa mapungufu hayo ambayo aliahidi kuyafanyia kazi.

Hata hivyo, Profesa Mgonda aliiomba Manispaa na Wizara ya Afya kuangalia adhabu hiyo waliyoitoa .
Baadhi
ya wagonjwa waliokuwa hospitalini hapo wakipata huduma walishtushwa na
kusikitishwa na kitendo hicho, lakini walikipongeza na kutaka kuwa
endelevu.

Mmoja
kati ya wagonjwa hao aliyejitambulisha kwa jina la Neema Kiwalo
alisema, ukaguzi huo unatakiwa kuwa endelevu ili kuendelea kufichua
madudu yaliyopo katika hospitali mbalimbali nchini.

Aidha,
Msemaji Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamwaja
alisema, endapo hospitali hiyo watatimiza masharti waliyopewa na Mganga
Mkuu wa Manispaa wao kama wizara watafanya ukaguzi kuona kama
wamekamilisha.

Alisema
ikiwa watakuwa wamerekebisha kasoro hizo zilizopelekea kufungiwa
hospitali hiyo itaruhusiwa kutoa huduma zake kama kawaida.

hiyo imefungiwa wakati kukiwa kuna sakata linalokihusisha chuo chake,
kinachodaiwa kutupa viungo vya binadamu jalalani.

Katika
sakata hilo lililovuta hisia za watu na kuzua mjadala mitaani, katika
vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii, watu wanane wakiwemo
madaktari wa IMTU, walikamatwa na Polisi kwa mahojiano wakituhumiwa
kuhusika katika utupaji viungo vya binadamu jalalani.

Serikali
wakati ikiendelea kuchunguza tukio hilo ikiwemo kuunda tume nyingine ya
watu 15 chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kujiridhisha kabla
ya hatua kuchukuliwa iliyopewa siku saba kukamilisha kazi yake, tume
hiyo imeundwa kukiwa na tume nyingine iliyoundwa na Polisi Kanda Maalumu
ya Dar es Salaam.

Tume
iliyoundwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
imejielekeza kuja na majibu kadhaa, ikiwa ni pamoja na kufahamu idadi
kamili ya watu wenye viungo hivyo.

Ikiwa
na watu saba akiwemo Mkemia Mkuu wa Serikali, Tume hiyo itakuja na
majibu yanayofafanua viungo hivyo ni vya muda gani na zilitumika
kemikali gani kuvikausha.

Pia,
jopo hilo litabaini kama ipo sheria na ni ipi inavunjwa. Wataalamu hao
wanalenga kubaini, pia kama upo uzembe katika kulinda viungo vya
binadamu na vinapatikanaje kwa ajili ya mazoezi.

mujibu wa Polisi, mifuko ipatayo 85 yenye vichwa, miguu, mikono, moyo,
mapafu, vifua na mifupa ya aina mbalimbali ya binadamu, ilikutwa maeneo
ya bonde la Mbweni Mpiji eneo la Bunju jijini Dar es Salaam.

No comments:
Post a Comment