Rose Ndauka akiwa na mumewe, Malick Bandawe
Staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka
hivi karibuni aliamua kumkimbia mumewe Malick Bandawe, kisa mfungo wa
Ramadhani ambapo sasa anaishi Kigogo na mama yake mzazi.
Akipiga stori na paparazi, Rose alisema
amelazimika kwenda nyumbani kwao ili kumpisha mumewe atimize nguzo hiyo
ya Uislam bila kipingamizi kutokana na kutokufunga ndoa.
“Mimi sifungi hivyo nimeona pia ni jambo
la busara kumpa nafasi mwenzangu kwa ajili ya kufanya ibada hiyo, mwezi
ukiisha nitarudi na maisha yetu yataendelea kama kawaida,” alisema Rose
ambaye awali alikuwa akiishi na mumewe huyo Tandale jijini Dar.
No comments:
Post a Comment