Thursday, 3 July 2014

Ridhiwani akana kujihusisha na biashara ya madawa pamoja na kumiliki magari ya UDA





5_1Mbunge
wa Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete
amekana kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya pamoja na kuwa
miongoni mwa watu ambao wanamiliki mabasi ya UDA.








Ridhiwani amekana hayo leo kupitia
ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live
kinachofanyika kila siku ya Jumatano kupitia ukurasa huo.




Ridhiwani alisema kuwa anasikitishwa na
kuumizwa na watu wanaofanya biashara ya madawa ya kulevya kwa kuwa
yamekuwa yakiathiri vijana kwa namna mbalimbali na pia alikana kuhusika
na biashara ya mafuta na gesi pamoja na kumiliki kampuni ya mabasi
inayomiliki mabasi ya UDA.

No comments:

Post a Comment