Saturday, 5 July 2014

Mlipuko mkubwa umetokea na milio ya risasi imeripotiwa karibu Bunge la Somalia





somalia2




Mlipuko mkubwa umetokea na milio ya risasi imeripotiwa karibu Bunge la Somalia wakati wabunge wakiwa katika kikao chao.
Kwa mujibu wa BBC, Ripoti za awali
zinasema kuna watu kadhaa wamejeruhiwa kutokana na mlipuko huo
unaosemekana umesababishwa na bomu lililolipuka kwenye gari.
somalia
Watu kumi walikufa wakati kundi la
kiislamu la wapinganaji la Somalia Al Shabaab waliposhambulia jengo la
bunge wiki sita zilizopita.
Kundi la Al shabaab lilipoteza udhibithi
katika mji mkuu wa Mogadishu tangu mwaka 2011 na tangu wakati huo
limekuwa likiendesha mashambulizi ya mabomu na kufanya mauaji.
Mapema wiki hii Mbunge maarufu Ahmed
Mohamud Hayd, aliuawa kwa kupigwa risasi katika mji huo, katika
shambulio linalodaiwa kufanywa na Al Shabaab.

No comments:

Post a Comment