Saturday, 5 July 2014

Mbasha akielezea mchungaji Gwajima alivyotembea na mkewe na njama ya kumfunga





Emmanuel Mbasha ambaye ni mume wa mwimbaji wa injili
maarufu, Flora Mbasha ameandika barua ndefu iliyobeba mengi yanayohusu
sakata lilizua uhasama kati yake na Mchungaji Gwajima kuhusu mkewe.



Mbasha amabaye hivi sasa anatuhumiwa kwa kesi ya ubakaji amedai kuwa
hata kesi yake ni sehemu ya njama za mchungaji huyo juu ya mkewe.



Hata hivyo, Mbasha amemtumia ujumbe mkewe na kueleza imani yake kuwa ipo siku watarudiana.



Isome hapa:



“Mchungaji…yapata kama wiki mbili zilizopita nilihoji kupitia
vyombo vya habari juu ya ‘utajiri’… wa ghafla wa mke wangu Mara baada ya
mgogoro kutokea kati yangu na yeye, bila kupoteza muda mkewangu
akanijibu kupitia gazeti moja la udaku kuwa amechangiwa fedha kiasi cha
milioni 9 na waumini kanisani kwakoMchungaji, naomba uelewe kuwa
nafahamu juu ya mipango yote mnayoipanga kuliko unavyodhani!!




Kwanza ni kweli kuwa mlipitisha harambee ya kumchangia mkewangu,
lakini kiwango kilichopatikana kilikuwa ni milioni 2 na laki tatu na si
milioni tisa kama mlivyotangaza!! Lakini mlitangaza uongo huo makusudi
iwe rahisi kutimiza malengo yenu ya kidhalimu mliyoyapanga juu
yangu!!Mnamo tarehe 3 mwezi juni mwaka huu, mlifungua akaunti mpya kwa
jina la mkewangu katika benki ya crdb morogoro, na siku nne baadae
mkewangu aliingiziwa fedha kiasi cha milioni 18 kutoka akaunti ya
MWANAMAPINDUZI FOUNDATION ambayo hyo accnt ipo nmb mwanza! Ambapo asasi
hii inamilikiwa na mchungaji wako msaidizi Maximilian Machumu pamoja na
mbunge wa viti maalumu kutoka mikoa ya kaskazini!




Nashukuru kama ulimpa fedha hizi kwa nia ya kumsaidia, lakini
hofu yangu ni kuwa kwanini kitendo hiki kifanyike kwa kificho?? Kwanini
mtumie njia za siri ambazo si rahisi watu kujua kama mmempa fedha??




Pia napatwa na mashaka zaidi kwani siku moja baada ya fedha hizi
kuingizwa taarifa ya benki inaonyesha kuwa kiasi cha milioni sita cash
zilitolewa na siku hiyo hiyo wapo waandishi watatu wa magazeti ya udaku
ambao wanaonekana waliingiziwa fedha kiasi cha milioni moja kila mtu na
aliyedeposit hizo fedha ni moja ya viongozi wako hapo kanisani!! Kuna
nini hapo??




Mchungaji, naomba tusizunguke mbuyu! Ni dhahiri shahiri kuwa umekuwa na uhusiano wenye utata na mkewangu kwa muda mrefu sasa!



Binafsi nilianza kupata wasiwasi mwaka jana mwezi desemba
tulipoenda katika mkutano wako wa injili pale morogoro! Mimi na mkewangu
tulifikia hoteli ya kingsway msamvu na wewe ulifikia Nashera Hotel
maeneo ya forest hill!! Baada ya siku tatu za mahubiri mkutano wako
ulipigwa marufuku na serikali kwasababu ya maneno yakichochezi uliyokuwa
unahubiri, hvyo ikatulazimu waimbaji wote turejee dar es salaam!!




Lakini uliniomba mkewangu abaki na wewe kwani ulipanga uwe
unawafanyia watu maombi pale kanisani kwako kihonda kwa muda wa siku
nne!! Nilikubali na nikamuacha mkewangu nyumbani kwa dada yako pale
mazimbu!! Lakini kesho yake dada yako alisafiri kwenda mwanza na ikabidi
mkewangu arudi hotelini kingsway!!




Kwaa taarifa nilizonazo na nimezithibitisha kupitia wahudumu wa
pale hotelini ni kuwa mkewangu hakuwahi kulala pale hata siku moja
ingawa chumba kililipiwa kwa siku zote zile!! Unaweza kunijibu alikuwa
analala wapi?? Je unaweza kunieleza kwanini mkewangu alikuwa analetwa
nashera hoteli na taxi kila siku usiku!! Sibahatishi katika hili kwani
hata namba ya dereva taxi ninayo!!




Yote haya nilivumilia, na hapa kati kati kuna mengi sana
yametokea lakini nikajifanya mjinga nikajishusha nikavumilia kwa lengo
la kulinda ndoa yangu isiharibike lakini naona wenzangu hambadiliki wala
hamjishitukii sana sana mapenzi ndio yanzidi kuwa motomoto kati yenu!!
Ulikuwa unategemea nivumilie mpaka lini, nijishushe kiasi gani, niwe
mjinga kiasi gani Nilikuvumilia sana mchungaji lakini sasa imefika point
hapana, imetosha lazima nikuondelee uvivu watanzania na dunia ikufahamu
jinsi ulivyo na kitendo ulichonifanyaia na unataka kuniziba mdomo kwa
kunitishia jela miaka 30!!!




Wewe ni mpuuzi na shetani anaishi ndani yako… na nataka nikuahidi
kitu kimoja kuwa NITAKUSHINDA! Najua utanisumbua sana kutokana na hela
zako but at the end, I will be the last man standing!! Narudia tena,
nitakushinda.!! Bila kusahau naomba niongee na wewe pia mkewangu, hivi
ni nini kilichokukuta ndani ya moyo wako How did we get here?? Je ni
fedha zilizokufanya ukengeuke kiasi hicho au kuna kingine?? Kama
unanichukia mimi kiasi hiki je, uwahurumii hata watoto wetu?? Mbona
tunawatengenezea mikosi wakiwa wadogo hivi?? Hivi unadhani watoto
wanajisikiaje watakaposikia kuwa baba ameenda jela kwa kosa la kubaka
lakini aliyechongesha muvi yote hiyo ni mama?? Hivi kisaikolojia hawa
watoto watakuwaje Si watakuwa huku wanatuchukia sisi wote wawili kwa
aibu na mikosi hii tunayowatengenezea Kwanini tunataka kuwataabisha
watoto kwa dhambi ambayo hawajaitenda.




Yes nafahamu nimekukosea mengi and am very sory for that, lakini
basi embu kumbuka mkewangu nimekuvumilia mambo mangapi mkewangu, kumbuka
makosa mazito uliyonifanyia lakini nikakusamehe ni sijamsimulia hata
ndugu yako ama ndugu yangu ili kulinda heshima yako!! Kumbuka jinsi
tulivyopogana na changamoto mbalimbali mpaka leo hii umefikia kuwa moja
ya icons wa muziki wa injili hapa nchini?? Kumbuka shida, manyanyaso,
dhuluma, kuchekwa na kudharauliwa ambako tumepitia mpaka leo hii tuko
hapa!!!




Mkewangu, kwa miaka yote hii nimekubali nionekane bushoke tu huku
watu hawajui kuwa mimi ndiye ninayechora ramani ya kila ishu yako!!
Mimi ndiye nimekuwa nafatilia na kufanikisha kila kitu chako from
scratch!!! Lakini nimekubali jamii inione bushoke kwani nilikuwa najua
nini mimi na wewe tunatengeneza kwa maisha yetu ya sasa na baadae!!!
Nini kilichokubadilisha mkewangu Fedha Au huyo mchungaji
mwanamazingaombwe.




Hivi kweli kabisa umefikia hatua ya kulipa waandishi wa habari
ili wanikandamize nionekane sifai katika jamii Ni nini kilichokuoata
mkewangu?? Naomba uelewe kuwa binafsi siogopi kwenda jela kwasababu ya
hiyo muvi mliyonizushia, kwani ni bora nikakae jela kuliko kuishi huru
huku mkininyanyasa kiasi cha kuondoa utu wangu kama bidamu, lakini
kinachoniuma ni familia yetu!! Kwanini watoto wateseke kwa sababu ya
tamaa zetu binafsi!! Nikifikiria hilo naumia sana!




Najua kwa sasa inaonekana kama vile ni impossible kwa mimi na
wewe kurudiana tena, lakini binafsi naamini tunaweza!! Najua haitakuwa
rahisi kwani tumeharibu mno, lakini ni heri ya kujaribu kuliko kuendelea
kufanya huu upuuzi tunoufanya sasa!! Kumbuka hiki tunachokifanya sasa
hatujajipaka matope sisi tu pekee, bali mziki wote wa injili Tanzania,
na tusipotubu tukajirudi Mungu atatuhukumu kwa dhambi hii!!




Kumbuka kuwa hakuna kati yenu atakayeshinda katika hii vita,
vyombo vya habari pekee ndivyo vitakavyo nufaika lakini mimi, wewe na
mchungaji wote tuta loose!! Mwisho nimalizie na wewe mchungaji,
tulipokutana mara ya kwanza nilikuchukulia kama kaka na kama mlezi wetu
wa kiroho!! Lakini umegeuka shetani mwenye pembe saba, umeparaganyisha
familia yangu, umeleta maumivu makali kwenye ukoo!!




Nakuonya tena kwa mara nyingine, muache mkewangu!! Huyo ni
mkewangu, nilimtolea mahali mimi mwenyewe na wazazi wake waliniamini na
kunikabidhi!!! Nasema niachie mkewangu!!




Wewe ni nyoka, imefika time watanzania wakujue ukweli wako wewe
mbwa mwitu mkali uliyevaa ngozi ya kondoo!!! Umedanganya watu vya
kutosha na umefarakanisha ndoa nyingi sana kwa sababu ya kiburi cha pesa
zako chafu za sembe!! Umeudhalilisha ulokole kiasi cha kutosha imefika
time tuwaeleze watanzania ukweli na wakufahamu kuwa wewe ni nyoka!!




Sitakubali kuona ukiendelea kuitesa familia yangu, nitapambana na
nitakushinda!!! Siogopi fedha zako wala connection ulizonazo, ni bora
nife nikiwa nimesimama kuliko kuishi nimepiga magoti! Nitapambana na
wewe mpaka mwisho ili historia isomeke vizuri ili hata wanangu wakiwa
wakubwa wajue kuwa baba yao sikuwa lofa kiasi cha kupiga magoti na
kuelekeza shingo kibla kuruhusu mdhalimu kama wewe uichinje familia
yangu, bali licha ya umasikini wangu nilisimama kiume na kupigana
kutetea familia yangu!!!




Narudia tena mchungaji, nitapambana na nitakushinda…”Kwako- Mchungaji Gwajima.”

No comments:

Post a Comment