YULE mwanamke anayejulikana kwa jina la
Amina Said Maige ambaye anakesi ya kumng’ata na kumchoma kwa pasi
hausigeli wake, Yusta Kashinda (20), ameachiwa kwa dhamana.
Amina alisomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Mohamed Salum mbele ya Hakimu Mkazi, Yohana Yongolo.
Mahakama imemuachi kwa dhamana baada ya
masharti yake ya kuwapata waajiriwa wawili pamoja na kiasi cha shilingi
milioni tatu kila mmoja kukamilika.
Amina alikamatwa Juni 4 mwaka huu na
kufikishwa Kituo cha Polisi Oysterbay kwa kupatikana na kosa la
Kumng’ata, kumchoma kwa pasi na kumpiga mwili mzima, Yusta.
Kesi yake ipo katika Mahakama ya Wilaya
ya Kinondoni, Dar ambapo mara ya kwanza alisomewa mashtaka Juni 12 na
kesi kuhairishwa mpaka Juni 26 pamoja na Julai 10.
Kesi yake itasomwa tena Julai 22 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment