Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa
amesema madai kwamba yeye ni tajiri hayana ukweli wowote. Amesema yeye
ni mfugaji na anamiliki ng’ombe zaidi ya 800 katika Jimbo la Monduli,
mkoani Arusha.
Lowassa alisema hayo katika mahojiano maalumu yaliyofanyika ofisini kwake wiki iliyopita mjini Dodoma.
“Haya madai hayana hata chembe ya ukweli
hata kidogo, isipokuwa mimi nadhani wananitakia mema kwa sababu ukiona
jumba zuri wanasema la Lowassa, gari nzuri la Lowassa, kitu chochote
kizuri wanasema cha Lowassa,” alisema na kuongeza:
“Wamesema uongo mwingi sana, mimi nasema
tu nilichopata nimepata na sina utajiri kiasi hicho, lakini si
mbadhirifu wa haki zangu ninazopata kama mshahara na haki nyingine.”
Alipotakiwa kutaja mali anazomiliki, Lowassa alisema: “Mimi ni mfugaji, nina ng’ombe zaidi ya 800 jimboni kwangu Monduli.”
Lowassa ambaye pia ni mbunge wa Monduli,
alisema madai kwamba anamiliki utajiri uliopindukia yalianza kabla
hajajiuzulu uwaziri mkuu na ilielezwa kuwa “maduka fulani” ni yake.
Alibainisha kuwa hata kampuni ya
Alphatel ambayo wanamiliki kwenye familia yake iliwahi kuhusishwa na
jengo kubwa lililojengwa na mtu mmoja mwenye asili ya Kiasia wilayani
Kinondoni, Dar es Salaam likiitwa Alpha.
“Ikaonekana ni jengo langu, kule Mbezi
kuna rafiki yangu mmoja walienda watu wakasema hii nyumba ya Lowassa.
Yule bwana alitoka na bastola akawakimbiza. Mimi sina nyumba maeneo
hayo,” alisema Lowassa.
Chanzo: Mwananchi.
No comments:
Post a Comment