Vikosi
vya serikali Somalia vimefanikiwa kuidhibiti upya ikulu ya rais katika
mji mkuu Mogadishu baada ya hapo awali wapiganaji wa kiislamu
kuishambulia.
Maafisa
wanasema washambuliaji wapatao watano kutoka kundi la al-Shabab
waliuawa walipoingia katika eneo la ikulu hiyo.Washambuliaji hao
wanadaiwa kulipua bomu lililotegwa kwenye gari karibu na langu kuu la
Ikulu hiyo.
Waziri
wa habari na mawasiliano wa Somalia Mustaf Dhuhulow ameambia BBC kuwa
tayari mmoja wa washambuliaji hao amekamatwa na anahojiwa na polisi.
Waziri
Mustaf amesema, '' Walishambulia ikulu ya rais saa za jioni. Alikuwa
watu washambuliaji watatu pamoja na dereva wao. Washambuliaji hao
waliuawa lakini dereva wao alipata majeraha madogo na anazuiliwa na
polisi na kuhojiwa. Walijaribu kuvamia Villa Somalia lakini
wakakomeshwa. Tutawapa maelezo zaidi baadaye. Na tutaweza kutoa maelezo
zaidi kwa raia wa Somalia na dunia nzima.''
Shambulio la Al shabaab Mogadishu
Hii
ni mara ya pili kwa Al Shabaab kuvamia ikulu ya rais mjini Mogadishu
mwaka huu japo mara ya kwanza walifanikiwa kuingia ndani.Rais Hassan
Sheikh Mohamoud hakuwepo wakati wa shambulio hilo.
Kundi
la wapiganaji wa kiislamu Al shabaab limefukuzwa kutoka mjini Mogadishu
tangu mwaka wa 2011 lakini limekuwa likifanya mashambulio ya kuvizia
tangu wakati huo.
Wanamgambo
hao wanaaminiwa kufanya mashambulio kadhaa pia katika nchi jirani ya
Somalia kama vile Kenya, Uganda na Tanzania kama njia ya kulipiza kisasi
kwa kuingia majeshi ya Umoja wa Afrika nchini Somalia.
No comments:
Post a Comment