Kama ulikuwa Hewani siku ya jana katika kipindi maarufu kabisa (XXL), ndani ya Stetion maarufu hapa Tz yaana nazungumzia CLOUDS Fm utaelewa nini ninachozungumzia mpaka sasa.
Katika hali isiyotegemewa jana watangazaji watatu maarufu kama, DJ FETTY, ADAM MCHOVU na B12 walizichapa ndani ya studio za Clouds live huku wakisahau kuwa Wasikilizaji wanawasikia mwanzo mwisho wanachokifanya huko ndani ya studio.
Sakata hilo limesababisha na kutoelewana baina ya hawa watangazaji juu ya mauzo ya Albam ya Fiesta!
Sasa leo watu mbalimbali na wasikilizaji
walikuwa nataka kujua nini zaidi kilitokea kupitia kipindi cha
Hekaheka, chanzo cha ugomvi hasa ni nn?
Baada ya massage nyingi sana kwenye
kipindi cha hekaheka ilibidi wahusika wanyanyue simu zao kuwatafuta
Adam, Fetty na B12 kujua nini kilichosababisha kuchapana makonde wakati
bado kipindi kikiwa hewani. Muhusika alinyanyua moja kwamoja simu na
kumpigia B12 ambaye alikataa kabisa kueleza chanzo cha sakata hilo la
kutwangana huku akisema mambo yote yapo kwa uongozi.....
![]() |
| PICHA YA STUDIO ZA CLOUDS BAADA YA KUZICHAPA |
Simu
ya pili ilimuendea ADAM MCHOMVU ambaye pia aligoma kuelezea
kilichotokea jana, baada ya Muda mfupi Adam alimkabidhi Dem wake ili
azungumze na mwandishi, huku akijua kwamba harikodiwi kumbe yupo hewani,
alikiambia kipindi cha hekaheka kwamba ADAM amemaind na hataki kuongea
na simu!!
Simu ya tatu ilienda kwa DJ FETTY, Ambapo iliita bila majibu kwamba ilikuwa haipatikani..
Chanzo kinasema kwamba baada ya ugomvi,
vifaa mbalimbali vya studio vimeharibiwa wakati wa ugomvi huo kama MIC,
COMPUTER Meza nk. Endelea Kufuatilia Hapa ili ujua ni hatua Gani
watachukuliwa watangazaji hawa kwa kukosa utovu wa Nidhamu....
SIKILIZA UGOMVI HUO LIVE HAPA CHINI
http://www.hulkshare.com/millard_ayo_/kilichotokea-kwenye-xxl-june-02

No comments:
Post a Comment