Wanawake CCM wamfariji Vicky Kamata baada ya harusi yake kukwama…
Wabunge wanawake wenye muda mrefu
bungeni pamoja na mke wa waziri mkuu, Mama Tunu Pinda juzi walimuandalia
sherehe ya kumfariji mbunge wa viti maalum (CCM), Vicky Kamata baada ya
harusi aliyotarajia kufunga wiki iliyopita, kukwama.
Sherehe hiyo ya faraja, ilifanyika Hoteli ya Dodoma kati ya saa 1.00 jioni na saa 6.45 usiku juzi mjini hapa.
“Unajua hata yeye mwenyewe
tulim-surprise (tulimshtukiza). Alijua kuwa ni chakula cha jioni, lakini
alipofika alikutana na muziki, kwaya na wabunge wengine waliompokea kwa
vifijo na nderemo,” alisema mmoja wa wabunge waliohudhuria hafla hiyo.
Sherehe hizo zilitumbuizwa na kwaya ya kikiristo ya Mvuke ya kanisa la
Anglican mjini Dodoma.
Alisema Vicky alijua kuwa amealikwa na
mbunge wa viti maalum (CCM), Magreth Sitta kwa ajili ya chakula cha
jioni lakini alipofika aka kutana na sherehe.
“Tuliona ni vyema kumuandalia sherehe
kidogo ili kumpa moyo kwamba hayo yametokea kwa sababu Mungu alitaka
kumuepushia na mambo makubwa siku za usoni,” alidokeza mmoja wa
waliohudhuria sherehe hiyo.
Baadhi ya wabunge waliohudhuria ni
wabunge wa viti maalum kutoka CCM ambao ni Magreth Sitta, Anna Abdallah,
Felister Bura, Hilda Ngoye, Agness Hokororo na Anastazia Wambura.
Wengine waliohudhuria ni Asumpta Mshama
(Nkenge-CCM), Anne Kilango (Same Mashariki-CCM) na Waride Bakari Jadu
(Kiembe Samaki-CCM). Chanzo hicho kilisema wabunge Anne Kilango, Magreth
Sitta na Anna abdallah, walielezea jinsi baadhi ya wanawake viongozi
walivyokumbwa na mikasa kama ya Vicky na wengine hata kuacha wakiwa
makanisani.
“Wengine walieleza jinsi walivyoteswa na
wenza wao na kwamba amshukuru Mungu pengine amemuepushia mambo makubwa
ambayo yangeweza kutokea kama ndoa ingefungwa,”alisema shuhuda huyo.
Alisema sherehe hiyo ilikuwa kama ibada
maana muda mwingi ulitumika katika kumuhubiria Vicky na kumsihi
asikatishwe tamaa na badala yake asonge mbele.
Alipoulizwa kuhusu sherehe hiyo, Vicky alikiri kufanyika lakini akakataa kuielezea kwa kina.
“Mimi niliitwa kwenye chakula cha jioni
lakini nilipofika pale nistaajabu kukutana na sherehe,”alisema Vicky
ambaye alikataa kuelezea kwa kina kuhusu sherehe hizo.
No comments:
Post a Comment