Mtoto
Fatuma Hassan (9) anyedaiwa kufungiwa ndani kwa siku tatu kisha
kuchomwa moto mikononi na mama yake mkubwa aliyetajwa kwa jina moja la
Diana (38), mkazi wa maeneo ya Tandale.
Tukio hilo lilitokea Juni 10, mwaka huu
katika maeneo hayo ya Tandale Sokoni ambapo mama huyo alikuwa akiishi na
mtoto wa mdogo wake kwa kile kilichodaiwa kuwa alimchukua kwa ahadi ya
kumsomesha lakini kuna madai kuwa badala ya kufanya hivyo, alimnyanyasa.
Mama mkubwa wa mtoto Fatuma Hassan anyetuhumiwa kumtesa mtoto huyo.
Taarifa zilidai kwamba mama huyo aliamua
kumfanyia ukatili mtoto huyo akidai kuwa alichukua fedha hizo akiwa na
mwanaye wa kumzaa kwa ajili ya kwenda kutumia kununulia sambusa na juisi
shuleni.
Ilisemekana kwamba kitendo hicho
kilimkera mama huyo na kuamua kuwasubiri warudi ili awaulize kama kweli
walichukua fedha hizo ambapo walikiri kuzitumia shuleni.
Wakizungumza na paparazi, majirani wa
eneo hilo walisema kuwa walimuona mtoto Fatuma akipigwa na mama’ke huyo
mkubwa fimbo na kumchoma moto mikononi pasipo kumpeleka hospitali huku
akimpa onyo kali na kumfungia ndani.
Walisema kuwa mwanamke huyo amekuwa akimfungia ndani na kwenda kwenye genge lake.
Mjumbe wa eneo hilo, Said Sundi na Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Pakacha, Ally Mdee wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Wananchi walifikia hatua ya kufananisha
tukio hilo na lile la mtoto aliyefungiwa kwenye boksi mkoani Morogoro,
Nasra Mvungi (marehemu), walimkamata na kupiga simu katika Kituo cha
Polisi cha Magomeni ambapo askari walifika na kumchukua mwanamke huyo.
Pia walimpeleka mtoto Fatma kwenye
Hospitali ya Magomeni anakopatiwa matibabu huku mwanamke huyo
akishikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano na alifunguliwa kesi ya
kujeruhi yenye jalada namba MAG/RB/5676/2014.
No comments:
Post a Comment