Tuesday, 24 June 2014

TAZAMA PICHA- WAREMBO (WASHIRIKI) SHINDANO LA MISS SHINYANGA 2014 WATOA MSAADA WA CHAKULA KITUO CHA WATOTO WENYE ULEMAVU CHA BUHANGIJA MJINI SHINYANGA







Hapa ni katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga ambapo leo Warembo 20 wanaoshiriki shindano la kutafuta mrembo wa
mkoa wa Shinyanga(Miss Shinyanga 2014) wakiongozwa na mwandaaji wa Mashindano
hayo bi Asela Magaka wa Asela Promotions   
wametembelea
kituo  na kutoa msaada wa vyakula huku wakichangia kidogo walichokuwa
nacho kwenye mifuko yao kuchangia ujenzi wa bweni katika kituo hicho
chenye watoto zaidi ya 260.Pichani ni baadhi ya warembo wakiwa na baadhi
ya watoto wenye ulemavu wa ngozi wakionesha upendo
Watoto
wenye ulemavu waoishi katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha
Buhangija mjini Shinyanga wakiwa na baadhi ya washiriki wa shindano la
Miss Shinyanga 2014
Warembo
hao 20 wametembelea kituo hicho cha kulelea watoto wenye ulemavu wa
ngozi,wasioona na wasiosikia ikiwa ni katika maandalizi yao ya shindano
la kutafuta mrembo wa mkoa wa Shinyanga(Miss Shinyanga 2014)
litakalofanyika Juni 28,214 mjini Kahama,ambapo Mzee Yusuph akiwa
amembatana na wasii wengine kibao watatoa burudani siku hiyo,Katika hali
ya pekee shindano hilo litatanguliwa na shindano la kutafuta mrembo
mwenye kipaji mkoa wa Shinyanga(Miss Talent Shinyanga) kesho Juni
25,2014 katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambapo mwimbaji wa taarabu
Isha Mashauzi atakuwa akitoa burudani
Misaada iliyotolewa na Asela Promotions na  kukabidhiwa kwa mkuu wa
 kitengo cha Walemavu katika kituo cha Buhangija Jumuishi mwalimu
 Bright Mduma ni pamoja na,chumvi katoni 1, mchele kilo 100,unga wa sembe kilo
200,sukari kilo 20,mafuta ya kupikia lita 10,unga wa ngano kilo 50 na sabuni za unga za kufulia kilo
30, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 506,700/=.
Watoto wenye ulemavu wakiwa katika eneo la tukio leo
Aliyesimama ni mkuu
wa  kitengo cha Walemavu katika kituo cha
Buhangija Jumuishi mwalimu  Bright Mduma akizungumza wakati wa kupokea
msaada wa chakula kutoka Asela Promotions,ambapo alisema miongoni mwa
changamoto zilizopo katika kituo hicho ni upungufu wa mabweni ambapo
watoto wanalazimika kulala zaidi ya mmoja kitanda kimoja.Kulia ni
mwandaaji wa Shindano la Miss Shinyanga na Miss Talent Shinyanga 2014 bi
Asela Magaka  akiwa ameshika tama baada ya kupewa taarifa kuhusu hali
ngumu ya maisha wanayoishi watoto wenye ulemavu
Aliyesimama
Mkuu wa kitengo cha Walemavu kituo cha Buhangija
mwalimu Bright Mduma aliwashukuru washiriki wa shindano la Miss
Shinyanga kwa kuona umuhimu wa kufika katika kituo hicho ili kuona hali
halisi ya maisha ya watoto wenye ulemavu katika kituo cha Buhangija
Jumuishi mjini Shinyanga
Aliyesimama
ni mwandaaji wa Mashindano ya Miss Shinyanga mwaka 2014 bi Asela Magaka
kutoka Asela Promotions,ambaye amekuwa akifanya maandalizi ya Mamiss
Tangu mwaka 1999 akizungumza leo katika kituo cha kulelea watoto wenye
ulemavu cha Buhangija mjini Shinyanga.Magaka alisema ameamua kuwapeleka
warembo hao katika kituo hicho ili
kujua mambo yanaoendelea katika jamii ikizingatiwa kuwa kauli mbiu ni
“Urembo,
sanaa na jamii” hivyo ni vyema wakajua kuwa urembo unahusiano na mambo ya jamii,wajue
jamii inahitaji nini,na umuhimu wa kusaidia jamii,hii itasaidia warembo hawa
kuwa mabalozi wazuri katika kusaidia watu mbalimbali  wenye mahitaji
maalum katika jamii
.


Kushoto ni mlezi wa warembo(Matron) bi Asha saidi
Aliyesimama
ni bwana Mustapha Ramadhani ambaye ni mwalimu wa Mamiss kanda ya ziwa
akizungumza katika kituo cha Buhangija ambapo kufuatia changamoto ya
mabweni aliahidi kuchangia mfuko 1 wa saruji kwa kuungana na Warembo 20
wanaoshiriki wa shindano la Miss Shinyanga 2014 kuchangia mifuko 18 ya
saruji kwa ajili ya  kuchangia ujenzi wa bweni
la wavulana lililoanza kujengwa 2013 na Miss Tanzania mwaka 2012 Brigette
Alfred.
Baada
ya kufika katika kituo hicho cha kulelea watoto wenye ulemavu,baadhi ya
washiriki wa shindano la Miss Shinyanga 2014 walijikuta wakitokwa na
machozi na kuiomba serikali kuwachukulia sheria mara moja watu
wanaohusika na mauaji ya albino na kuitaka jamii kubadilika na kuacha
dhana ya kwamba watapata utajiri kupitia viungo vya albino
Bwana
Shaban ambaye pia ni mwalimu wa Mamiss kanda ya ziwa akizungumza mawili
matatu katika kituo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi,wasioona na
wasiosikia cha Buhangija mjini Shinyanga.Pamoja na mambo mengine
aliahidi kutoa kilo 20 za ngano kwa ajili ya watoto hao
Baadhi
ya washiriki Miss Shinyanga 2014-Kushoto ni bi Nyangi Warioba kutoka
Msalala kulia ni bi Mary Emmanuel kutoka Ushetu ambao waliguswa na
maisha ya watoto wenye ulemavu na kusababisha watokwe na machozi na
kuamua kuchangia mifuko miwili ya saruji kuchangia ujenzi wa bweni
lililoanza kujengwa na Miss Tanzani mwaka 2012 Brigette
Alfred.Warembo wote 20 wameahidi kuchangia mifuko ya saruji kwa ajili
ya ujenzi huo ikiwa ni kukamilisha mifuko 18 ya saruji
Kushoto
ni mwandaaji wa shindano la Miss Shinyanga 2014 bi Asela Magaka kutoka
Asela Promotions akikabidhi vyakula(moja ya mifuko ya unga wa sembe)
kwa mkuu wa  kitengo cha Walemavu katika kituo cha Buhangija Jumuishi mwalimu  Bright Mduma
Katikati ni Yasinta kwa niaba ya watoto wenye ulemavu wa  katika kituo cha Buhangija akipokea unga wa sembe 
Mwakilishi
wa watoto wenye ulemavu Yasinta akizungumza kwa niaba ya watoto wenzake
baada ya kupokea zawadi ya chakula kutoka kwa washiriki wa shindano la
Miss Shinyanga wakiongozwa na Asela Promotions ambapo aliwapongeza kwa
kitendo hicho na kuongeza kuwa  hivi sasa wanayo changamoto ya upungufu
wa Shuka na magodoro
Mmoja
wa washiriki wa shindano la Miss Shinyanga 2014 bi Nicole Sarakikya
kutoka Kishapu akiwa na watoto wenye ulemavu wakifuatilia kilichokuwa
kinajiri-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga




Habari kamili soma hapa chini
 Zikiwa zimesalia siku chache tu kabla ya kufanyika
shindano la kutafuta Mrembo wa mkoa wa Shinyanga,leo warembo 20 wanaoshiriki
shindano hilo wakiongozwa na mwandaaji wa Mashindano hayo bi Asela Magaka
(Asela Promotions) wametembelea kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha
Buhangija katika manispaa ya Shinyanga na kutoa msaada wa vyakula sambamba na
kuchangia mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa bweni katika kituo hicho.
Misaada iliyotolewa ni pamoja na,chumvi katoni 1, unga wa ngano kilo 50,mchele kilo
100,unga wa sembe kilo 200,sukari kilo 20,mafuta ya kupikia lita 10 na sabuni
za unga za kufulia kilo 30 vyote vikiwa na thamani ya shilingi 506,700/=.
Akikabidhi msaada huo wa chakula  kwa mkuu wa  kitengo cha Walemavu katika
kituo cha Buhangija Jumuishi mwalimu  Bright Mduma mwandaaji wa shindano la
Miss Shinyanga 2014 na Miss Talent Shinyanga 2014 bi Asela Magaka  kutoka
Asela Promotions amesema ameamua kuwapeleka warembo hao katika kituo hicho ili wajue
mambo yanaoendelea katika jamii ikizingatiwa kuwa kauli mbiu ni “Urembo, sanaa
na jamii”.
“Tunao wajibu wa kujua namna jamii inavyoishi,urembo
lazima uende sawa na jamii,nimewaleta washiriki wa miss Shinyanga 2014 ili
wajue kuwa urembo unahusiano na mambo ya jamii,wajue jamii inahitaji nini,na
umuhimu wa kusaidia jamii,hii itasaidia warembo hawa kuwa mabalozi wazuri
katika kusaidia watu mbalimbali  wenye mahitaji maalum katika
jamii”,aliongeza Magaka.
Katika hatua nyingine Magaka alieleza
kukerwa na tabia ya baadhi ya watu katika jamii wanaoua watu wenye ulemavu kwa
kuamini kuwa watapata utajiri na kuwataka waache vitendo hivyo kwani kwenda
kinyume na haki za binadamu kwa sababu kila mtu ana haki ya kuishi na mwenye
uwezo wa kutoa uhai wa binadamu ni mungu pekee.

Kwa upande wao washiriki wa shindano la
Miss Shinyanga 2014 ambao baadhi yao walijikuta wakitokwa na machozi waliiomba
serikali kuwachukulia sheria haraka iwezekanavyo wahusika wa mauaji ya watu
wenye ulemavu wa ngozi badala ya kila mara kusema Uchunguzi unaendelea
Naye  mkuu wa
kitengo cha walemavu kituo cha Buhangija mwalimu Bright Mduma amemshukuru
mwandaaji wa shindano la mrembo wa mkoa wa Shinyanga 2014 kwa kuona umuhimu wa
kusaidia watoto hao na kuwaomba washiriki wa shindano hilo kuwa mabalozi katika
jamii kuhamasisha mashirika,taasisi na watu mbalimbali wenye mapenzi mema
kujitokeza kuwasaidia watoto hao.
Aidha  Mduma amesema kituo cha kulelea watoto cha Buhangija cha
mjini Shinyanga hivi sasa kinalea watoto 36 wasioona,48 wasiosikia na wenye
ulemavu wa ngozi 180 huku changamoto ikiwa ni mabweni kwani sasa wanalazimika
kulala watoto zaidi ya mmoja kitanda kimoja ambapo mabweni mawili yanahitajika
kwa ajili ya watoto wa kiume na moja kwa watoto wa kike.
Kufuatia changamoto ya mabweni,
warembo hao 20 wanaoshiriki  shindano la Miss Shinyanga 2014 wakiongozwa
na mwandaaji wa Shindano hilo litakalofanyika terehe 28,Juni,2014 waliahidi
kuchangia mifuko 18 ya saruji kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa bweni la
wavulana lililoanza kujengwa 2013 na Miss Tanzania mwaka 2012 Brigette Alfred.
Jumla ya shilingi 80,000/=
zilipatikana papo hapo na kukabidhiwa kwa mkuu wa kitengo cha walemavu mwalimu
Bright Mduma,kwa ajili ya mifuko ya saruji miwili kati ya 18 waliyoahidi na
kubakiza mifuko 16 katika ahadi yao kuchangia ujenzi wa bweni hilo.
Ziara ya washiriki wa shindano
la mrembo wa mkoa wa Shinyanga 2014 imefanyika ikiwa wapo katika maandalizi ya
shindano hilo litakalofanyika Juni 28,mwaka 2014 mjini Kahama ambapo kabla ya
Shindano hilo kutafanyika shindano la kutafuta mrembo wa mkoa mwenye kipaji
litakalofanyika Siku ya Jumatano Juni 25,2014 mjini Shinyanga.

No comments:

Post a Comment