TAARIFA MPYA KUHUSU TAREHE YA KUWASILI KOCHA MAXIMO
Maandalizi
ya msimu wa ligi kuu ya Tanzania yameanza kupamba moto huku vilabu
vikijaribu kujiimarisha tayari kwa mapambano, kwa upande wa klabu ya
Yanga wameanza kwa kuimarisha benchi la ufundi kwa kumuajiri kocha
Marcio Maximo.
Kocha
huyo mbrazil anayeheshimika zaidi nchini, Marcio Maximo atatua Jangwani
ndani ya siku nne kuanzia leo Jumamosi. Bosi huyo ambaye anasifika
zaidi kwa msisitizo wake katika nidhamu za wachezaji atatua Jumanne
ikiwa ni mapema kabla ya uchaguzi wa Simba utakaofanyika Juni 29 Jijini
Dar es Salaam. Mwanaspoti linajua kwamba Maximo yuko jijini Brasilia
akifanya kazi ya uchambuzi wa mechi za Kombe la Dunia kwenye televisheni
ya Taifa ya Mexico na mkataba wake unamalizika Jumatatu.
Yanga
imethibitisha kwamba Maximo ameshaanza maandalizi ya safari hiyo tangu
juzi ambapo katika hilo pia amewajulisha baadhi ya maofisa wa Ubalozi wa
nchi hiyo nchini kuwa atakuwa Tanzania mapema wiki hii kumalizia
maongezi yake na mabosi wa Yanga.
Yanga
wamemleta Maximo mapema kufanya maandalizi ya uhakika katika kikosi cha
timu hiyo ikiwa ni kuwawahi wapinzani wao wa jadi Simba ambao bado wapo
katika mchakato wa uchaguzi.
“Ilikuwa kuna baadhi ya viongozi waende Brazil kumalizia mazungumzo na kusainishana mkataba lakini hilo limebadilishwa.
Maximo ndiyo atakuja Dar es Salaam kuepuka gharama,”alisisitiza mmoja wa viongozi wa Yanga.
No comments:
Post a Comment