Jacqueline Wolper akiwa kazini.
TABIA ya staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper kubadilibadili dini mara kwa mara imeonekana kuwakera watu mbalimbali akiwemo Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum ambaye amemcharukia vikali.
Wolper
kiimani ni Mkristo lakini hivi karibuni alibadili na kuwa Muislam kabla
ya kurejea tena kwenye imani yake ya awali ya ukristo.
Sababu
ya Wolper kubadili dini ilikuwa ni kufunga ndoa na aliyekuwa mchumba
wake Abdallah Mtoro ‘Dalas’, walipoachana akaamua kurudi kwenye ukristo.
Akizungumza
na paparazi juzikati, Shehe Salum, alisema Wolper anapaswa kujichunguza
na kubadilika haraka kwani kitendo anachofanya ni kinyume na taratibu
za dini.
“Siyo vizuri hata kidogo na hata dini zote zinakemea kitendo cha kuchezeachezea dini kwani ni chukizo kwa Mungu.
“Siyo vizuri hata kidogo na hata dini zote zinakemea kitendo cha kuchezeachezea dini kwani ni chukizo kwa Mungu.
“Kwa
upande wa Dini ya Kiislamu, kuna sheria kali zaidi kwa mtu akionekana
na tabia hiyo, anaweza hata kuuawa hivyo wanaofanya mchezo huo waache
kwani siyo vizuri. Huko ni kumfanyia Mungu dhihaka,” alisema Shehe Salum
na kuongeza:
“Unajua
suala la imani ni kitu kinachomhusu mtu binafsi, ni vyema kufanya
uamuzi wa hakika na kushika njia moja na siyo kufanya dhihaka na dini ya
Mwenyezi Mungu. Ni kitu kibaya sana.”
“Dini
siyo kitu cha kuchezea, ni daraja la kumfikisha mtu kwenye haki, si
mahala pa kuingia na kutoka, kuingia na kutoka. Huko ni kucheza na
Mungu. Namshauri huyo mtoto (akimaanisha Wolper) abadilike. Asifanye
mchezo na imani, Mungu anaweza kumlaani kwa kumchezea,”
No comments:
Post a Comment