Picha na maelezo ya bomu LA KIPINDI CHA vita ya Msumbiji lililoonekana Mtwara jioni ya Juni 16 BAADA YA KUOKOTWA NA WATOTO
Hili ni bomu ambalo jioni ya June 16 2014 kwenye kijiji cha Mdui kata ya Mawala wilaya ya Mtwara vijijini kwenye mkoa wa mtwara liliokotwa na watoto waliokuwa wakicheza karibu na eneo la makaburi.
Taarifa ilitolewa Polisi baadaye ambapo baada ya wataalamu kuja na
kuchunguza waligundua ni bomu la kurusha kwa mkono ambalo lina namba TNT
MORTAR BOMB 60MM,LOT SOL 618 ambapo Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la
Wananchi walichukua hatua za kiusalama na kwenda kulilipua porini.
Kaimu kamanda wa Polisi Mtwara Maisha Maganga alikuwa na haya ya kusema kuhusiana na bomu hilo:
"Ukiliangalia ni bomu ambalo ni la muda mrefu nadhani ni kipindi
kile cha vita ya Msumbiji, tulilipeleka porini likalipuliwa na ulipuaji
wake haukuwa na madhara… na sio kwamba ni bomu tunaweza kusema
limeletwa ama imekuaje, ni bomu la muda mrefu tu"




No comments:
Post a Comment