OHARI: BAADA YA VIFO, WASANII TUMENYOOKA
MKONGWE kwenye
sanaa za Kibongo, Blandina Chegula ‘Johari’ amesema kufuatia vifo vya
mfululizo vya wasanii, kwa kiasi kikubwa wasanii wamebadilika kitabia.
Akipiga
stori na paparazi alisema, wasanii hao wamejitambua kuwa duniani watu
wanapita, jambo ambalo kwa muda mrefu walikuwa wamelisahau na kuponda
raha mfululizo.
“Tangu
wenzetu wafariki mfululizo, wasanii wengi tumepata mshtuko na
kujitambua, naona wengi wamebadilika, wamenyooka na kuanza kumrudia
Mungu,” alisema Johari.
Vifo vya wasanii vilivyotokea hivi karibuni ni pamoja na cha Adam Kuambina, Sheila Haule ‘Recho’ na George Tyson.
Vifo vya wasanii vilivyotokea hivi karibuni ni pamoja na cha Adam Kuambina, Sheila Haule ‘Recho’ na George Tyson.
No comments:
Post a Comment