Wednesday, 4 June 2014

Naibu Waziri wa habari,Vijana, Utamaduni na Michezo awataja Nay wa Mitego, Shilole, Wema na Aunt Ezekiel kati ya wasanii waliopewa onyo na serikali



Naibu
Waziri wa habari,Vijana, Utamaduni na Michezo awataja Nay wa Mitego,
Shilole, Wema na Aunt Ezekiel kati ya wasanii waliopewa onyo na serikali




Ukiukwaji wa maadili ni sehemu ya kilio cha jamii ya
watanzania na tayari kilio hicho kimeifikia serikali ambayo imechukua
hatua za awali ya kuwaonya watu wanaofanya tabia hizo.


 

Naibu Waziri wa habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Juma Nkamia
ameeleza hatua ambazo wizara hiyo imechukua katika kukomesha ukiukwaji
wa maadili unaofanywa hasa katika kumbi za starehe.


 

Akijibu swali lililoulizwa na mbunge Catherine Magige, Nkamia amesema
kuwa serikali imefanya vikao na wamiliki wa kumbi za starehe, wamiliki
wa bendi,  maafisa wa utamaduni, na wakuu wa polisi.




  Amesema serikali imezuia kutoa vibali kwa vikundi vya ‘Kangamoko’
kutokana na uchezaji wake kutofuata maadili na kutoa mfano wa wasanii
ambao wamepewa onyo.


 

“Mfano wasanii waliopewa onyo ni Nay wa Mitego, Shilole na Anti Ezekiel. Na kwa upande wa kumbi ni Mamas &Papas.” Amesema

 

Naibu waziri huyo ameeleza kuwa serikali imeunda kamati ya kitaifa
yakuzuia ukatili, unyanyasaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi na watoto
na pia udhalilishaji wa wanawake.

No comments:

Post a Comment