Mzee Majuto:Wakati mwingine nachekesha si kwa kupenda bali huwa najikuta tu nafanya hivyo
Mchekeshaji wa muda mrefu Amri Athuman 'Mzee Majuto' ametoa kali ya mwaka baada ya kusema kuwa maisha yake ni komedi tosha kutokana na kumvunja mtu mbavu bila kujali yuko mahala gani....
Akizungumza
na paparazi, Mzee Majuto alisema yeye hutoa shoo muda wowote
bure bila kujali yuko katika wakati gani kwani maisha yake
ni komedi tupu...
"Maisha
yangu ni komedi tosha,siwezi kuacha kuchekesha.Wakati mwingine
si kwa kupenda bali huwa najikuta tu nimefanya hivyo , inabidi
watu wanizoee tu....
"Huwa
sina nia ya moja kwa moja kuchekesha watu, lakini kumbe kauli
zangu huwavunja mbavu.Sijisikii vibaya kwa hilo, najivunia
kuendelea kuwa msanii ninayekubalika hadi umri huu," alisema mzee Majuto

No comments:
Post a Comment