Jeneza lenye mwili wa marehemu Nasra
Rashid likibebwa kuingiza katika chumba cha kuhifadhia maiti cha
hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro ukitokea Dar es Salaam ambako
mtoto huyo alilazwa kwa matibabu zaidi kutokana na kuishi katika boksi
kwa kipindi cha miaka minne tangu kuzawaliwa kwake. PICHA/MTANDA BLOG.
NASRA ENZI ZA UHAI WAKE.
Kutokana na ratiba iliyotolewa na
viongozi wa ustawi wa jamii mwili wa Nasra utatarajiwa kuwasiri uwanja
wa jamhuri kuanzia majira ya saa 2 asubuhi na wakazi wa Manispaa ya
Morogoro na vitongoji vyake watapata fursa ya kuaga kisha saa 5 asubuhi
hiyo hiyo msafara utaelekea katika makaburi ya Kolla kwa ajili ya
mazishi.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Jole Bendera anatarajia kuwaongoza wananchi kuaga mwili huo.

Mhudumu wa chumba hicho cha kuhifadhia maiti akiwa amefungua jeneza ili kutoa mwili tayari kwa kuhifadhi katika jokofu.
Mama Mlezi wa Nasra Josephine Joel na
Mwandishi wa habari wa gazeti la habarileo Agnes Haule wakiwa kwenye
huzuni mara baada ya mwili huo kuhifadhi katika chumba cha
maiti.PICHA/MTANDA BLOG
Mwandishi wa habari wa gazeti la habarileo Agnes Haule wakiwa kwenye
huzuni mara baada ya mwili huo kuhifadhi katika chumba cha
maiti.PICHA/MTANDA BLOG
Baba mzazi wa Nasra (aliyeshika shavu) Rashid Mvungi akisikiliza jambo eneo la uwanja wa chumba cha kuhifadhia maiti.
Hapa akionekana mwenye huzuni kutokana na tukio hilo.
Mama Mlezi wa Nasra Josephine Joelakizungumza jambo na waandishi wa habari.
Akiteremka katika gari baada ya msafari uliobeba mwili wa marehemu mtoto wake Nasra kuwasili eneo hilo.PICHA/MTANDA BLOG.
Mtoto Nasra Rashid Mvungi (4),
aliyefichwa kwenye boksi kwa miaka minne, amefariki dunia katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na katika saa zake za mwisho za uhai
wake alisikika akitamka maneno “sitaki waje kunichukua”.

Nasra ambaye
alikuwa akitibiwa MNH, alifariki dunia usiku wa kuamkia jana baada ya
hali yake kubadilika Alhamisi iliyopita, kiasi cha kuhamishiwa katika
chumba cha uangalizi maalumu (ICU) ambako aliwekewa mashine ya kumsaidia
kupata hewa ya oksijeni.
Mama mlezi wa Nasra, Josephine
Joel alisema kabla hajawa mahututi, mtoto huyo alikuwa akiweweseka kwa
kuzungumza maneno mengi hali iliyosababisha wauguzi kumfanyia ibada
maalumu.
“Sitaki waje kunichukua, sitaki, sitaki, wasije
kunichukua, bibi Nasra umesikia,” ni maneno aliyokariri mlezi huyo
ambayo yalikuwa yakirudiwarudiwa na Nasra saa chache kabla ya hajawa
mahututi na kupelekwa ICU.
Josephine alisema mtoto huyo pia
kila mara alikuwa akidai apewe chips na soda na kwamba hadi mauti
yalipomkuta alikuwa akitibiwa maradhi ya homa ya mapafu ‘nemonia’.
“Nasra
alifariki saa 7.30 usiku, tangu Alhamisi iliyopita hali yake
ilibadilika na kuwa mbaya na imeendelea kuwa hivyo hadi alipofariki
dunia,” alisema na kuongeza:
“Bado niko Muhimbili nawasubiri
watu wa ustawi wa Jamii kutoka Morogoro wao ndiyo watakuwa na uamuzi
kuhusu mazishi ya mtoto huyo,” alisema.
Ofisa Habari wa MNH,
Aminiel Eligaeshi alithibitisha kifo cha mtoto huyo, ambaye alipokewa
hospitalini hapo Mei 26 mwaka huu akitokea Morogoro na kwamba hali yake
ilibadilika ghafla juzi saa 2:00 usiku.
“Jitihada za madaktari zilifikia kikomo saa 7:30 usiku, baada ya mtoto huyo kupoteza maisha,” alisema.
Kuzikwa kishujaa
Ofisa ustawi wa jamii Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungatuti amsema kuwa mazishi ya Nasra yatatanguliwa na ibada itakayoambatana na
utoaji wa heshima za mwisho katika Uwanja wa Jamhuri kesho, hatua ambayo
alisema inatokana na baba mzazi wa mtoto huyo, Rashid Mvungi kuwa mmoja
wa watuhumiwa wa mateso yake.
No comments:
Post a Comment