Meriam akiwa na mwanaye Maya, kushoto ni mumewe Daniel Wani aliyempakata mtoto wao wa kiume Martin na wadau waliopigania mama huyo kuachiwa huru kabla ya kukamatwa tena
Mwanamke Meriam Ibrahim aliyeachiwa huru juzi baada ya kuhukumiwa kifo kwa kosa la kuolewa na mwanamume mkristo na kukana dini ya kiisilamu amekamatwa tena akiwa na mumewe pamoja na watoto wawili katika uwanja wa ndege mjini Khartoum, Sudan.
Meriam amekamatwa na watu takribani 40 waliokuwa wamevalia mavazi ya
kiraia ikiwa ni masaa machache baada ya kuachiwa huru kutokana na uamuzi wa
mahakama ya rufaa.
Inadaiwa kuwa Meriam aliyejifungulia jela alikuwa anajiandaa kuondoka nchini Sudan pamoja na familia yake.

No comments:
Post a Comment