MTOTO ATEKETEA KWA MOTO NDANI.

Mtoto
mwenye umri wa miaka Mitatu na nusu aliyefahamika kwa jina la Rehema
Patrick, amefariki dunia baada ya chumba alichokuwa amelala kuteketea
kwa moto, hapo jana Mtaa wa Ilomba, jijini Mbeya.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, amethibitisha kutokea kwa ajali
hiyo na kuongeza kuwa chanzo cha moto huo hakijafahamika ambapo mtoto
huyo ambaye ni marehemu alikuwa amelala wakati mama yake mzazi
aliyefahamika kwa jina la Winfrida Sokon (30), alikuwa ameenda kuchota maji huku naye baba yake akiwa safarini.
R.I.P Rehema
No comments:
Post a Comment