Thursday, 5 June 2014

MSANII AMANDA YAMKUTA YA MAREHEMU RECHO


MSANII AMANDA YAMKUTA YA MAREHEMU RECHO

MWIGIZAJI mwenye figa ya aina yake Bongo Movie, Tamrina Posh ‘Amanda’ ameamka na kushtuka akiwa amechanjwa chale na watu wasiojulikana kama alivyowahi kufanyiwa marehemu Recho.

Akizungumzia tukio hilo, Amanda alisema lilitokea siku ambayo dairekta mkongwe nchini George Tyson alipofariki dunia (Mei 30) ambapo hakujua ni nani aliyemfanyia ‘unyambilisi’ huo usiku kwani alishtuka asubuhi na kuona akivuja damu zikiashiria kuchanjwa kwa wembe.

“Nilijikuta nimechanjwa lakini Mungu ni mwema, waliofanya hivyo kama walikuwa na nia mbaya, wameshindwa kwani nilikwenda kuombewa kanisani halitanipata lolote,” alisema Amanda.

No comments:

Post a Comment