MBASHA AANZA KUFIRISIWA: ALIZWA HATI ZA NYUMBA, VIWANJA PAMOJA NA KADI YA GARI..HABARI KAMILI HAPA
MAJANGA! Siku chache baada ya kuachiwa
kwa dhamana katika kesi ya kudaiwa kumbaka shemejiye, mwimbaji wa Injili
na mfanyabiashara Bongo, Emmanuel Mbasha amedaiwa kuibiwa hati za
nyumba na viwanja.
“Mbasha hakukuta kitu pale nyumbani, vilikombwa vyote sijui na nani. Inauma sana kwani mtu ndiyo kwanza ametoka mahabusu halafu anakuta nyumbani kwake hakuna vitu muhimu kama hivyo, inasikitisha sana,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo makini kilichomo ndani ya
familia, kimedai kuwa mara baada ya Mbasha kujitokeza na kuwekwa
mahabusu Juni 17, mwaka huu, mtu asiyejulikana alikwenda nyumbani kwa
mfanyabiashara huyo, Tabata-Kimanga, Dar na kukwapua hati za nyumba na
viwanja mbalimbali anavyovimiliki.
“Mbasha hakukuta kitu pale nyumbani, vilikombwa vyote sijui na nani. Inauma sana kwani mtu ndiyo kwanza ametoka mahabusu halafu anakuta nyumbani kwake hakuna vitu muhimu kama hivyo, inasikitisha sana,” kilisema chanzo hicho.
Kikizidi kumwaga data, chanzo hicho
kilisema katika vitu vilivyoibwa ni pamoja na nyaraka mbalimbali
zikiwemo hati za viwanja kadhaa vilivyopo Iringa, kadi ya gari na vitu
vingine vidogovidogo.

msichana aliyedai kuwa amebakwa na mbasha
Baada ya kunyaka madai hayo,paparazi tulimtafuta Mbasha ili kujua ukweli wa ishu hiyo ambapo alipopatikana alikiri kutovikuta vitu hivyo muhimu nyumbani kwake.
“Ni kweli kama ulivyosikia ila nisingependa kuzungumzia kila kitu kwa sasa nahitaji kupumzisha akili,” alisema Mbasha.

Mbasha aliyetoka kwa dhamana Juni 19,
katika kesi hiyo ya kudaiwa kubaka iliyosomwa katika Mahakama ya Wilaya
ya Ilala, kesi yake itatajwa tena Julai 17, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment