MAMA ZITTO; aliteseka kwa miezi tisa kabla ya kifo chake.
Rais
Kikwete alipokwenda kumjulia hali mama mzazi wa Zitto Kabwe, Bi. Shida
Salum Mohamed alipokuwa ICU kwenye Hospitali ya Ami, Masaki, Dar es
Salaam.
Shida
ambaye ni mama mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto
Zuberi Kabwe, alianza kusumbuliwa na maradhi ya saratani ya shingo ya
kizazi Agosti, mwaka jana, ingawa hali yake ilimpa afadhali nyakati
kadhaa.
Hata
hivyo, tulimebaini kuwa hata kabla ya Agosti mwaka jana, Shida aliwahi
kuzidiwa na maradhi ambapo Zitto alimpeleka India kwa matibabu, ingawa
haijafahamika wakati huo alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa gani.
Kwa
mujibu wa Zitto, baada ya Shida kuugua Agosti mwaka jana, alipatiwa
matibabu kisha hali yake iliimarika na kuanza kufanya shughuli zake za
kawaida.
“Tulikuwa na matumaini makubwa sana kwa wakati huo kwa jinsi maendeleo yake yalivyokuwa lakini Februari mwaka huu ghafla mambo yalibadilika,” alisema Zitto.
“Tulikuwa na matumaini makubwa sana kwa wakati huo kwa jinsi maendeleo yake yalivyokuwa lakini Februari mwaka huu ghafla mambo yalibadilika,” alisema Zitto.
MASKINI HAKUWEZA KUAPISHWA KUWA MBUNGE WA KATIBA
Mapema mwaka huu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, alimteua Shida kuwa mmoja kati ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba katika kundi la 201 kutokana na nafasi yake ya uenyekiti wa Chawata.

ambaye ni mwanachama wa Chadema, vilevile mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya
chama hicho, alikwenda Dodoma Februari mwaka huu kwa ajili ya kuhudhuria
vikao vya Bunge Maalum la Katiba lakini wakati anasubiri kuapishwa hali
yake ilibadilika.
Zitto
alimwambia paparazi kuwa baada ya hali ya mama yake kubadilika,
alipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako alianzishiwa
matibabu kabla ya kusafirishwa kwenda India kwa matibabu zaidi.
Alisema, baada ya kutoka India aliendelea kutibiwa nyumbani katika kipindi ambacho hali yake ilikuwa na nafuu lakini ilipobadilika tena, alipelekwa Ami ambako alitibiwa mpaka mauti yalipomkuta.
Alisema, baada ya kutoka India aliendelea kutibiwa nyumbani katika kipindi ambacho hali yake ilikuwa na nafuu lakini ilipobadilika tena, alipelekwa Ami ambako alitibiwa mpaka mauti yalipomkuta.
MAZISHI KIGOMA
Mwili wa Shida, ulisafirishwa kwa ndege juzi alasiri na mazishi yalitarajiwa kufanyika jana mkoani Kigoma.
Viongozi mbalimbali kutoka vyama tofauti vya siasa, walikuwa bega kwa bega na Zitto kuanzia Hospitali ya Ami na baadhi walisafiri kwenda kushiriki mazishi ya Shida.
Baadhi
ya viongozi waliokuwa bega kwa bega na Zitto ni wabunge, Catherine
Magige, Grace Kiwelu, Edward Lowassa, Nimroad Mkono, Halima Mdee, Deo
Filikunjombe, Murtaza Mangungu, Ester Bulaya, Hamisi Kessy na wengine
wengi, huku maveterani wa siasa na taaluma nchini, Dk. Salim Ahmed
Salim, Profesa Philemon Sarungi na Profesa Issa Shivji wakishiriki
kikamilifu.Mwili wa Shida, ulisafirishwa kwa ndege juzi alasiri na mazishi yalitarajiwa kufanyika jana mkoani Kigoma.
Viongozi mbalimbali kutoka vyama tofauti vya siasa, walikuwa bega kwa bega na Zitto kuanzia Hospitali ya Ami na baadhi walisafiri kwenda kushiriki mazishi ya Shida.
Sisi Sote ni wa Mwenyezi Mungu na Kwake Sote Tutarejea.
No comments:
Post a Comment