Wednesday, 4 June 2014

MAJANGA:DEREVA NA UTINGO WAJIIBIA MALI WALIZOKUWA WAKISAFIRISHA KWENDA KONGO ZIKIWA NA THAMANI YA TSH MILIONI 100 ,WACHOMA LORI LILILOKUWA NA MZIGO HUO



MAJANGA:DEREVA
NA UTINGO WAJIIBIA MALI WALIZOKUWA WAKISAFIRISHA KWENDA KONGO ZIKIWA NA
THAMANI YA TSH MILIONI 100 ,WACHOMA LORI LILILOKUWA NA MZIGO HUO


Kamanda
 wa polisi  mkoa  wa Iringa Ramadhan Mungi kushoto akisalimiana na
mwakilishi wa kampuni ya Dandu ambao lori lao limeteketezwa kwa moto 
Kamanda
 wa  polisi mkoa wa Iringa akionyesha mitumba  iliyohifadhiwa katika
nyumba  moja Nyololo baada ya kufaulishwa na dereva na utingo wake kisha
lori kuchoma moto 
Hii ndio  mitumba  iliyohifadhiwa mali ya wizi 
Mitumba  hiyo ikionekana kwa nje baada ya kujaa ndani ya nyumba hiyo kupita kiasi 


RPC Iringa Ramadhan Mungi akiangalia  mitumba  iliyohifadhiwa porini baada ya  kuporwa 
kamanda
wa  polisi Iringa Ramadhan Mungi akimwonyesha mmiliki wa nyumba
iliyohifadhi  mali  hizo za wizi kulia na dereva wa gari hilo mbele
lenye namba  T 185 CJM ambalo  ndilo lilikuwa likisomba mali  hizo za
wizi kutoka katika  lori lililochomwa moto 

Mwonekano wa lori hilo kwa ndani baada ya mali zote  kuhamishwa kwa  lengo la kuziiba 
Hili
ndilo lori  lililokuwa na mali  hizo  chini kukiwa na ubichi wa mafuta
 ya taa yaliyomwagwa ili  kulilipua lori hilo bila mafanikio 

 
JESHI
la  polisi  mkoa  wa Iringa kupitia dhana ya polisi  jamii na ulinzi
shirikishi  limefanikiwa  kukamata  mali za wizi zilizokuwa 
zikisafirishwa kwenda nchi ya DRC Kongo zikiwa na thamani ya  Tsh
milioni 100 pamoja na lori  lenye thamani  ya Tsh milioni 100 ambalo
liliteketezwa kwa  moto kabla ya dereva na utingo wa  lori hilo 
kulichoma moto kama njia ya kupoteza ushahidi.

Imedaiwa 
kuwa  watu  zaidi ya 6  wanashikiliwa na  jeshi  hilo la polisi
akiwemo  dereva  na utingo  wake ambao wanadaiwa  kuhusika na tukio  la
wizi  huo.

Kamanda 
wa  polisi mkoa  wa  Iringa Ramadhan Mungi  alisema  kuwa  tukio hilo 
lilitokea juzi May 31 ambapo  askari  wa  doria  wilaya ya Mufindi 
wakiwa katika shughuli   hiyo ya doria  walifanikiwa  kuliona  lori
hilo  likiwa  limeegeshwa kando ya  barabara ya Iringa –Mbeya  eneo la
Kinegembasi wilaya ya Mufindi  huku likiwa  limeteketea kwa moto katika
kibini yake.

Alisema
kuwa  watu hao waliteketeza lori lenye namba za usajili  T527 DPQ
likiwa na tela lenye namba  T 974  EFE  aina ya  scania mali ya kampuni
ya Dandu ambalo  walilikuta  likiungua   huku silizi  zake zikiwa 
zimefunguliwa na  baada  ya uchungu wa awali  walibaini  kuwa lori hilo 
lilikuwa limebeba mitumba na viatu  na baada ya msako  ndipo 
walipofanikiwa  kukuta mitumba  hiyo  ikiwa imefichwa katika  nyumba
moja kuukuu mali ya mama  Gray Mpinga  mwenyeji wa Maguhani Mufindi.


Alisema 
kuwa mali  hizo ambazo ni mabelo ya mitumba na viatu  yalitoka
Bandarini kwenda DRC  chini ya  dereva wa  lori hilo ni Enedia Christian
(26) mkazi wa Mbeya  na utingo wake  Deus  Gendo (20) mkazi wa Mbeya .

Kamanda 
Mungi  alisema kuwa utingo na dereva wa  lori hilo baada ya kufika
kijiji  hicho cha Maguhani  walivunja kontena na  kushusha mali zote na
kuzihifadhi katika  nyumba   hiyo kabla ya  kutafuta mteja na kisha
 lori  kulichoma moto.

Alisema
kuwa  baada ya  kufanya  wizi huo  walitoweka na simu zao kuzimwa na
kutokana na jitihada za  jeshi la  polisi  kupitia mtandao wa
kimawasiliano wa kuthibiti na wizi  wa mitandaoni  walifanikiwa 
kuwanasa  watuhumiwa hao wakiwa kijiji cha Nyololo.

Mbali
ya kuwakamata  dereva na  tingo  pia  polisi  wamekamata  watu  mbali
mbali  wahusika  wa mtandao huo na kuendelea  kumsaka Masko Buhewa mkazi
wa Nyololo kwa  kuhusika na umilikiwa wa mtandao huo .

No comments:

Post a Comment