Mwili wa mtoto Nasra Mvungi ukishushwa kwenye gari ndani ya Uwanja wa Jamhuri Morogoro kuagwa.
Habari
zilizopatikana mjini hapa, zinasema kuwa mzozo umeibuka kwa ndugu wa
marehemu Nasra ambapo baba yake mzazi, Rashid Mvungi na bibi wa
marehemu, Asha Abdallah (mama mzazi wa mama wa marehemu ambaye pia ni
marehemu) kila mmoja akitaka kuuchukua mwili wa Nasra na kuuzika.
Nasra Mvungi, enzi ya uhai wake.
“Mjukuu
wangu nina uchungu naye sana, nakumbuka mengi sana kuhusu yeye. Nataka
kumzika mwenyewe. Hapa nilipo nimeshaagiza maturubai kwa ajili ya kuweka
msiba nyumbani kwangu,” alisema Bi. Asha kwa masikitiko.
Mwili wa mtoto Nasra Mvungi ukiwa tayari kuagwa Uwanja wa Jamhuri Morogoro.
TUliwasiliana
na Ofisa Ustawi wa Jamii, Mkoa wa Morogoro, Osward Ngungamtitu na
kumsimulia kuhusu mvutano huo wa kifamilia, ambapo alisema wao kama
chombo cha serikali ndiyo wanaohusika na msiba huo.
“Sasa
hivi (juzi Jumatatu saa 7 mchana) tunapita Chalinze, tunakuja na maiti
huko Morogoro. Sisi kama serikali kwa kuwa ndiyo tuliosimamia matibabu
ya Nasra, sisi ndiyo tutasimamia pia maziko yake. Wanatofautiana bure
tu.
Nasra Mvungi enzi ya uhai wake akiwa na baba yake mzazi Rashid Mvungi.
“Tutafikisha
maiti mochwari hapo Hospitali ya Mkoa halafu ataagwa katika Uwanja wa
Jamhuri kabla ya mazishi siku hiyohiyo (jana).”
No comments:
Post a Comment