Mmiliki wa Nyumba aliyokutwa Nyoka mkubwa na kuuwawa na wananchi wa sakina leo
June 05 2014 mchana kupitia mitandao mbalimbali Tanzania zilisambaa
taarifa zikimuhusu mmiliki wa mojawapo ya nyumba maeneo ya Sakina jijini
Arusha kwamba nyoka aliekua akimfuga kwa siku nyingi na kuhusishwa na
imani za kishirikina, ameuwawa na Wananchi.
Wananchi
walimuua nyoka huyo na kisha kumkata kata vipandevipande ambapo baada
ya hizi taarifa kusambaa mmiliki wa nyumba hii aliomba kuongea na millardayo.com ili kutoa maelezo yake ambayo anadai ndio ukweli wenyewe.
Mr.Joseph
Paschal Magesa anasema >>Mimi kama mimi kwanza ni Mkristo safi na
mzee wa kanisa na niliondoka nyumbani jana na mke wangu kutoka Arusha
kuelekea Dar es salaam, sijui lolote kuhusiana na hicho kitu ila
nilipofika maeneo ya Mwanga na Same nikapigiwa simu kwamba kuna nyoka
huku ndani ya eneo la garden nyumbani, kuna vijana niliwaacha wawili
pale nyumbani nikawaambia waambieni watu wawasaidie kumuua huyo nyoka’
‘Wakamuita
jirani yangu hapo ndipo nae akanipigia simu nikamwambia bwana wewe si
una bunduki nisaidie kumuua huyo nyoka ila alivyokata simu nilijua
ametekeleza kumbe aliondoka, baadae napiga tena simu nauliza vipi
naambiwa bado yupo na watu wamejaa nikawauliza kwani hao watu hawawezi
kumuua mpaka bunduki wakasema wanaweza ndio baadae wakanambia wamemvuta
mkia wamemuweka nje ya geti’
‘Nikawauliza
anavutika asije akawa analeta shida wakasema anavutika, nikawaambia
mpelekeni kanisani kwa sababu nyumbani kwangu ni jirani na kanisa ndio
wakamvuta hadi kanisani wakammwagia maji ya baraka kisha wakamkatakata
ndo ikawa mwisho wake hapo’.
‘Kusema
kwamba nilikua nafuga kwamba huyu nyoka ni mtoto wangu wa kwanza…..
sasa kama ni mtoto wangu wa kwanza si inamaana na mtoto wangu angekufa
na yeye? mimi nasema namwachia Mungu tu…….. sijawahi kusikia Nyoka
kuishi maeneo hayo toka nimeanza kuishi kwa karibu miaka 8, hata na mimi
inanitatiza manake nimetumiwa picha Nyoka amefungwa kitambaa chenye
maandishi mekundu kama ya kiarabuarabu hivi…..’
‘Taarifa
kwamba Nyoka huyu amevunja kioo cha dirisha akiwa anatokea ndani ya
nyumba, sio kweli…. haipo kabisa hiyo kitu eti kwamba ametokea ndani,
hayo ni mambo ya watu tu… hicho kioo nilikifunja mimi wakati napanga
mizigo ya ofisi yangu… sifahamu chochote kuhusu huyu Nyoka, Watanzania
waniamini haya ninayosema ndio yanayotoka moyoni mwangu’
CLICK >>HAPA<<
No comments:
Post a Comment