Tukio hilo lililoshobokewa na wanaume
wakware, lilitokea wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Meeda, Sinza –
Mori, Dar ambapo mkali huyo aliye Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo
‘Wazee wa Kizigo’ alikuwa akiporomosha shoo ya nguvu na kundi lake.
Muziki ulipokolea wadada hao waliokuwa
wamevalia nguo saresare walikwenda jukwaani na kuanza kucheza kabla ya
baadaye kuanza kujiachia kihasarahasara.
Madada hao wakicheza kwa furaha.
“Mh! Hawa wadada vipi? Mbona wanaleta
mambo ya Kanga Moko hapa? Cheza gani ile ya aibu namna ile...hawa lazima
ni machangu. Wamekosa wateja sasa wamekuja kumtega Choki, maana mambo
yale kama siyo machangu utawaitaje?” alisikika dada mmoja akisema
ukumbini humo.
Lakini hali ilikuwa tofauti kwa wanaume
wakware ambao kwao ilikuwa faraja kujionea mambo ya chumbani hadharani,
kwani walikuwa wakiwashangilia.
Hata hivyo, wakati wadada hao wakiendelea kufanya yao, Choki wa watu hakuwa na la kufanya, zaidi ya kuduwaa na kuwashangaa tu.
Ili kuonyesha kuwa vichwani mwao
hamnazo, wadada hao hawakuona haya kuachia maungo yao wazi, hata pale
makufuli yalipobaki nje, walionekana hawana habari kabisa.
Ilifikia mahali, mmoja wao akaenda mbali
zaidi baada ya kutaka kuvua nguo, hakupewa nafasi hiyo, mabaunsa
walimbeba na kumtoa ili wastaarabu waendelee kuburudika na Wazee wa
Kizigo.
No comments:
Post a Comment