JE, WAJUA?!MSIBA WA TYSON HUKO KENYA NI HATARI TUPU....!SOMA ZAIDI HAPA...
wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mwongoza filamu za Kibongo, marehemu
George Otieno Okumu ‘Tyson’ nchini kwao Kenya ni zaidi ya msiba.
Majonzi na simanzi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mwongoza filamu za Kibongo, marehemu George Otieno Okumu ‘Tyson’ katika Viwanja vya Leaders.
Tyson aliagwa na mastaa, mashabiki na wadau wa burudani Bongo kwenye
Viwanja vya Leaders Kinondoni, Dar kabla ya mwili wake kusafirishwa kwa
ndege kwenda Kenya kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika Kisumu nchini
humo keshokutwa Jumamosi.
Mbali na Wabongo, pia kulikuwa na Wakenya ambao walitumia nafasi hiyo
kumuaga mwenzao ambapo baadhi yao waliambatana na mwili huo kwenda
Kenya.
Baada ya kuagwa, mwili wa marehemu ulipelekwa kwenye Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar tayari kwa safari ya
Kenya.
Sonia na Monalisa wakiwa na nyuso za huzuni wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Tyson.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, mwili wa marehemu ulipokewa kwa majonzi
makubwa na ndugu, jamaa, marafiki, mastaa na watu mbalimbali kwenye
Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi nchini humo.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini humo hasa redio, mitandao
ya kijamii na ‘blogi’ vilieleza kwa simanzi kubwa juu ya kifo cha Tyson
kwani kabla ya kujikita Tanzania mwaka 2000 alikuwa akifahamika kama
bondia matata ndiyo chanzo cha kupewa jina la Tyson nchini humo.
Baadhi
ya vyombo vilivyoripoti na kusababisha Kenya kuzizima kwa vilio ni
pamoja na Radio Citizen, Citizen Television, mitandao ya Kenya.co.ke,
mseto.co.ke, Ghafla.co.ke na mingine kibao.
“Kusema kweli kwa hapa Nairobi, Tyson alikuwa akifahamika sana.
Unajua watu wengi walikuwa hawaamini lakini baada ya mwili kuwasili
ndiyo wameamini.
“Hata ndugu walikuwa hawaamini hadi walipoona jeneza na kuhakikishiwa
kuwa limebeba mwili wa mpendwa wao,” alisema shuhuda wetu kutoka Jiji
la Nairobi.
Baada ya kufikishwa Nairobi, ndipo taratibu za kuupeleka
mwili huo zikaanza ambapo utapumzishwa kwenye nyumba ya milele Kisumu
Jumamosi ijayo.
Tyson
alifanya kazi nyingi Bongo ikiwa ni pamoja na kufungua milango ya Bongo
Movies alipotengeneza kwa mara ya kwanza Filamu ya Girlfriend na
baadaye ikifuatiwa na Dilemma.
Pia alikuwa mwongozaji wa vipindi mbalimbali runingani kuanzia ITV,
EATV na TV1. Alipatwa na mauti maeneo ya Gairo, Morogoro baada ya
kutokea ajali mbaya akitokea Dodoma kutengeneza Kipindi cha Mboni Show
cha EATV chini ya mwanadada Mboni Masimba.
Wakati wimbi la vifo vya wasanii likiongezeka, katika hali ya
kushtua, mtabiri na mnajimu maarufu Bongo, Maalim Hassan Yahya Hussein
ameendelea kusisitiza kuwa utabiri juu ya vifo vya mastaa utaendelea
hadi mwezi Aprili, mwakani.
Akizungumza
na waandishi wa Global Publishers kwenye makao makuu ya gazeti hili
Bamaga-Mwenge jijini Dar, Maalim Hassan ambaye ni mtoto wa aliyekuwa
mnajibu Afrika na kwingineko duniani, marehemu Shehe Yahya Hussein
alisema:
“Nasisitiza tena, mwezi wa kinyota huanza Aprili na kuishia Aprili.
Katika kipindi cha mwaka huu, kinyota inaonesha watakufa wasanii
mfululizo hivyo ni vema wakachukua tahadhari na kukubaliana na hali
halisi.”
Alipoulizwa nini cha kufanya, Maalim Hassan aliendelea:
“Wasanii
wanatakiwa kumuomba Mungu. Kama ni Muislam asikose kuswali msikitini,
kama Mkristo asikose kuhudhuria kanisani na kama ni mpagani, basi
atafute namna yake ya kumuomba mungu wake.”
Mbali na Mungu, Maalim alikwenda mbele zaidi: “Pia kinyota wasanii
wasivae nguo nyekundu kabisa. Wasipake rangi nyekundu midomoni
(lipstick) na kwenye kucha zote. Kimsingi waachane na vitu vya rangi
nyekundu.
“Pia wasitoke kwenda kwenye starehe au shughuli za usiku hasa Jumanne
na Jumamosi jioni kwani ni siku za vita kati sayari ya Venus na Mercury
ambapo mkuu wake ni Israeli Mtoa Roho.”
Alisema kuwa suala la vifo vya wasanii si kwa Tanzania tu kwani hivi
karibuni tasnia ya filamu duniani imekuwa ikiondokewa na wasanii kibao
kuanzia Hollywood (Marekani),
Nollywood
(Nigeria), Bollywood (India) na hata nchini Kenya mwigizaji aliyeigiza
kama Idd Amin kwenye simema ya Rise and Fall of Idd Amin amefariki dunia
hivi karibuni hivyo ndiyo hali halisi kwa kipindi hiki hadi Aprili,
mwakani.<
Mbali na Tyson anga la bururudani Bongo liliwapoteza wasanii wengine
kama Shaila Haule ‘Recho’ Adam Philip Kuambiana na Amina Ngaluma.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. Amina.
No comments:
Post a Comment