Inatisha!!! KIJANA ALIYEPOTEA KISHIRIKINA APATIKANA AKIWA KATIKA HALI YA KUTISHA,AKUTWA NA MATOPE MWILI MZIMA HAJITAMBUI
Kijana mmoja mkazi wa kijiji cha Nyambogo wilayani Rorya mkoani Mara, ambaye anadaiwa kupotea nyumbani kwa imani za kishirikina hatimaye amepatikana huku akiwa katika hali ya kutisha bila kujitambua na mwili wake ukiwa umejaa tope jingi, tukio ambalo limevuta mamia ya wananchi wa kijiji hicho.
Kijana
huyo Kenedy oguko mwenye umri wa miaka 22 amekutwa nje ya nyumba yao
asubuhi ya Juni 5 mwaka huu akiwa uchi wa mnyama,ambapo baadhi ya
mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa tangu kutoweka kwa kijana huyo
siku nne zilizopita,wamekuwa wakimtafuta bila mafanikio huku wakihusisha
tukio hilo na imani za kishirikina.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rorya Bw Samwel Kiboye,ambaye
ni miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo amewaomba wananchi kuacha
kulipiza visasi kwa kuwasaka watu wanaotuhumiwa kwa ushirikina bali
watumie vyombo vya dola huku mwenyekiti wa kijiji hicho akilaani vikali
vitendo hivyo vya ushirikina vinavyoendelea kijijini hapo hatua ambayo
amesema imesabisha wananchi sasa kuishi kwa hofu kubwa.




No comments:
Post a Comment