INASIKITISHA: ABIRIA AFIA NDANI YA BASI
WATU
wawili wamefariki dunia mkoani Kilimanjaro katika matukio tofauti,
likiwemo la mmoja aliyekutwa amekufa akiwa katika basi la Kampuni ya
Kilenga akiwa safarini kuelekea mkoani Arusha.Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro, Moita Koka, alisema kuwa mtu huyo ametambuliwa kwa jina la
Sayuni Joel (53), mfanyabiashara, mkazi wa Mwembe, wilayani Same,
Kilimanjaro.
Akizungumzia
mazingira ya tukio hilo, Kamanda Koka alisema Joel alipanda basi hilo T
398 BAT na kwamba kabla ya kufikwa na mauti, alikuwa akisumbuliwa na
tumbo na alikuwa akielekea hospitali kupata matibabu.Alisema Joel
aligundulika kuwa amepoteza maisha baada ya gari hilo kuingia katika
stendi kuu ya mabasi Moshi.
Maiti
yake imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC huku uchunguzi wa
chanzo cha kifo hicho ukiendelea.Katika tukio jingine, mkazi wa Kijiji
cha Kilema – Kiyou, Kata ya Kilema, wilayani Moshi, Martin Michael (45),
amekufa baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya chandarua.
Mashuhuda
wa tukio hilo walisema lilitokea juzi, saa 8 mchana na kudai kwamba
amefikia uamuzi huo kutokana na kuchoshwa na hali yake kiafya ambayo
imemfanya kutumia dawa kila mara na kwamba kabla ya tukio hilo aliwahi
kusikika akilalamikia hali hiyo.
Na Dixon Busagaga, moshi

No comments:
Post a Comment