HII HAPA VIDEO NYINGINE AMBAYO HUENDA NAYO IKAFUNGIWA NCHINI KENYA....
Wiki
kadhaa zilizopita, Kundi la muziki la Sauti Sol la Kenya liliachia
video yake ya Nishike ambayo baadae ilifungiwa kuchezwa kwenye vituo vya
Televisheni kutokana na madai ya kutokuwa na maadili, Lakini sasa nae
mwanadada Sanaipei Tande ameachia Video ya wimbo wake unaotamba kwenye
vituo mbalimbali vya Radio Kenya “Mfalme Wa Mapenzi” ambapo tayari
mitandao imeanza kuandika kuhusiana na video na kusema iko mbioni
kufungiwa kutokana na maudhui yake.
Video
hiyo inaonyesha Scene mbalimbali za kimapenzi imeonekana kuwashtuka
watu wengi na kuwa gumzo kwenye mitandao ambapo tangu kuachiwa kwake
jana tu tayari imeangaliwa zaidi ya mara 16,000 katika mtandao wa
Youtube, swali ni Je itafanikiwa kuchezwa katika vituo vya Televisheni
nchini humo?
Itazame Video yenyewe hii hapa.
waweza pia kuicheck >>hapa<<
No comments:
Post a Comment