FIFA ZAANZA KUCHUNGUZA WAJERUMANI WALIOWABAGUA WAAFRIKA KATIKA SARE YA 2-2 DHIDI YA GHANA
Wamenaswa: Mashabiki wawili waliojipaka rangi nyeusi wakiwa katika pozi kwenye mchezo baina ya Ujerumani na Ghana.
SHIRIKISHO
la soka Duniani, FIFA linachunguza picha zilizozagaa zikiwaonesha
mashabiki wakiwa wamejipaka rangi nyeusi katika mchezo wa kundi G baina
ya Ujerumani na Ghana.
Picha
zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha wanaume wawili,
wanaoonekana kuwa mashabiki wa Ujerumani, wakiwa na sura nyeusi kwenye
uwanja wa Fortaleza jumamosi iliyopita.
FIFA imesema kamati yake ya maadili ipo katika majadiliano ya kufungua kesi.
Wanatazama mechi: Mashabiki wawili walinaswa na kamera katika sare ya 2-2 baina ya Ujerumani dhidi ya Ghana.
"Siku
zote tunachukua ushahidi wote na kuupeleka kamati ya maadili. Ni kamati
ya maadili itakayokutana," Msemaji wa FIFA amewaambia The Guardian.
"Kama kutaonekana kuna ukweli kesi itafunguliwa. Hilo lipo juu ya kamati
ya maadili, wao ndio watachukua maamuzi".
FIFA huwa wanayawajibisha mashirikisho ambayo mashabiki wake wanaonesha utovu wa nidhamu uwanjani.
Katika tukio la pili, mtu aliingia uwanjani kipindi cha pili wakati wa sare ya 2-2.
Mtu huyo ambaye hakuwa na shati aliripotiwa kuwa ni Mpoland na alijiandika namba za simu na anwani ya barua pepe tumboni kwake.
Kiungo
wa zamani wa Portsmouth na Sunderland, Sully Muntari, ambaye kwasasa
anacheza AC Milan alimsalimia mtu huyo kabla ya kuondolewa na maaskari
wa usalama.
Msemaji
wa kamati ya maandilizi ya Brazil, Saint-Clair Milesi alisema mtu huyo
aliingia kutokana na uzembe wa mamlaka zinazohusika na usalama uwanjani.
No comments:
Post a Comment