Tayari wamewashangaza mashabiki wao
kwa kuonyesha video ya harusi yao iliyofungwa mwaka 2008 na kuzaliwa kwa
mtoto wao Blue Ivy, sasa Beyonce na Jay Z wametoa mshtuko mwingine kwa
mashabiki wao kwenye ziara yao ya muziki ya On The Run inayoendelea.
Bey na Jay Z waliwaonyesha mashabiki
picha za mfululizo wa matukio yaliyomkumba mwanamuziki Justin Bieber
hivi karibuni huku Beyonce akitoa kauli kwa mashabiki kuwa “Even the
greatest can fall.”
Baadhi ya mashabiki walisema hiyo ni
diss kubwa kwa Bieber ambaye amekumbwa na matukio ya kukamatwa mara
kadhaa katika miezi ya hivi karibuni.
Mashabiki wengine walidai hiyo sio
heshima kwa Justin Bieber huku wengine wakiandika kupitia mitandao ya
kijamii kuwa hilo ni funzo kwake sio tusi.
No comments:
Post a Comment