Wednesday, 25 June 2014

Batuli: Sijawahi kula hela ya mume wa mtu na kamwe siwezi kuugeuza mwili wangu kuwa mtaji





Staa 
wa  kike  anayefanya  vizuri  katika  tasnia  ya  fillamu Yobnesh
Yusuph ‘Batuli’   amefunguka  na  kudai  kuwa  hajawahi  kula  hela  ya 
mume  wa  mtu  na  kama  watu  wanamhisi  hivyo  basi  watakuwa 
wanakosea  sana.....


Batuli 
alitoa  kauli  hiyo  ili  kuwathibitishia  mashabiki  wake  juu  ya 
kauli  mbovu  za  watu  kuwa  urembo  wake  unategemea  mtaji  wa 
mwili  wake  ambapo  amewajibu  kwa  kusema  kuwa    urembo  na  uzuri 
wake  unatokana  na  matunda  ya  kazi  yake  ya  sanaa  na  kimsingi 
anautumia  huko   kwa  kuwa  haoni  faida  ya  kula  hela  ya  mwanaume 
kwani  hajaifanyia  kazi.....

"Amini 
kuwa  naendesha  maisha  yangu  kwa  misingi  ya  kazi  zangu,
inawezekana  wapo  wanawake  wanaoishi mjini  kwa  kutegemea  mtaji  wa 
miili  yao  na  si  sanaa.

"
Kwa  upande  wangu  hata  Mungu  ananiona  kuwa  kile  ninachokipata 
kupitia  sanaa  ndicho  ninachokitumia  kwenye  matumizi  yangu,"
alisema  Batuli


No comments:

Post a Comment