BALOZI IDDI AONGEA NA WANANCHI WA KIVUNGE NA TUMBATU KUHUSU MATATIZO YA UVUVI.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na wananchi wa
Kijiji cha Kivunge kuhusu hitilafu za uvuvi kati ya Kijiji hicho na
Tumbatu katika uwanja wa michezo wa Good Hope Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini
Unaguja. Kushoto ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Nd. Haji Juma haji na Katibu wa mkoa Huo Bibi Caterina.
Umati
wa wananchi wa Kivunge wakisikiliza nasaha za Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif hayupo pichani kwenye mkutano wa kutathmini
hitilafu iliyojitokeza ya uvuvi kati ya wananachi wa Kivunge na Tumbatu.
Mwakilishi
wa Wananchi wa Kijiji cha Kivunge Bwana Sharifu Kombo Sharifuakitoa
Taarifa ya tukio la kuchomwa moto kwa chombo cha Uvuvi cha wavuvi wa
Kijiji hicho Kisiwani Tumbatu Mapema Mwaka huu.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Nd. Haji Juma Haji akiwaasa wananchi wa
Kivunge kujiepusha na cheche zinazopenyezwa na baadhi ya watu kwenye
migogoro yao ya kijamii hapo uwanja wa michezo wa Good Hope Mkwajuni. Picha na Hassan Issa wa – OPMR – ZNZ.
****************************************************************
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameonya kwamba
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuanzia sasa haitachukuwa dhamana tena
ya kulipa gharama zozote zitakazotokana na baadhi ya watu kujichukulia
sheria mikononi mwao kwa kuvunjiana vyombo vyao wavyovitegemea katika
kuendesha maisha yao ya kila siku.
Alisema
kitakachosimamiwa zaidi kwa sasa katika kukabiliana na wimbi hilo
linaloonekana kuendelezwa katika baadhi ya maeneo hapa nchini ni
kufuatwa kwa mkondo wa sheria dhidi ya watu watakaohusika na uharibifu
wowote ule wa mali za raia au za Umma. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE




No comments:
Post a Comment