Tuesday, 3 June 2014

Audio: G-Unit yarudi tena! Waachia wimbo mpya 'Nah I'm Talking 'Bout', Usikilize hapa

Audio: G-Unit yarudi tena! Waachia wimbo mpya 'Nah I'm Talking 'Bout', Usikilize hapa




Siku moja baada ya kundi la G- Unit kuungana jukwani katika show ya Summer Jam iliyoandiwa na Hot 97, wasanii wote wanne walioiunda G-Unit ya awali wamekutana kwenye wimbo mmoja ikiwa ni baada ya miaka sita.
50 Cent, Lloyd Banks, Young Buck na Tony Yayo wameweka kando tofauti zao na wameamua kupiga kazi, ‘Nah I’m Talking Bout ni wimbo unaoirudisha ladha ya G-Unit kwa mashabiki.
Hii ni remix wimbo wa Hit-Boy na HS87 “Grinding’ My Whole Life” na wamempa shavu pia Kidd Kidd.
Je, ndo kurudi kabisa kwa kundi lile la zamani au ni ushirikiano wa wimbo mmoja?
“Everything cool here till trip.” Amesema 50 Cent kwa utani.
Leo (June 3) ni siku ambayo albam ya 50 Cent ‘Animal Ambition’ inatoka rasmi.

No comments:

Post a Comment