Friday, 30 May 2014

Taarifa Rasmi Kwa Umma Kutoka IKULU:Rais Jakaya Kikwete Alipowasili Toronto Canada kuhudhuria mkutano unaohusu Afya ya Mama na Mtoto kufuatia mualiko kutoka kwa Waziri Mkuu wa Canada Mheshimiwa Stephen Harper.



Taarifa
Rasmi Kwa Umma Kutoka IKULU:Rais Jakaya Kikwete Alipowasili Toronto
Canada kuhudhuria mkutano unaohusu Afya ya Mama na Mtoto kufuatia
mualiko kutoka kwa Waziri Mkuu wa Canada Mheshimiwa Stephen Harper.










 Rais Jakaya Kikwete
--

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewasili Toronto Canada tarehe 27 Mei,
2014 usiku  kuhudhuria mkutano unaohusu Afya ya Mama na Mtoto kufuatia
mualiko kutoka kwa Waziri Mkuu wa Canada Mheshimiwa Stephen Harper.



Mkutano wa Afya ya Mama na Mtoto , (Maternal, Newborn and Child Health -MNCH)
unaanza Leo tarehe 28 – 30 Mei, 2014 ambapo Rais Kikwete pia anatarajiwa kuwa
miongoni mwa wazungumzaji wakuu.



Lengo la mkutano huu ni kutoa nafasi kwa wataalamu na viongozi wa dunia kufikia
makubaliano kwa pamoja kuhusu jitihada na hatma kuhusu MNCH.



Mkutano huu unatarajiwa kutilia mkazo jitihada za kuimarisha huduma za afya,
kuweka kumbukumbu za taarifa, katika jitihada za kupunguza vifo vya mama na
watoto wachanga katika nchi zinazoendelea.



Mkutano huu unatarajiwa kuhudhuriwa na kiongozi wa Kidini, Mhe. Aga Khan,
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki Moon na Bibi Melinda Gates , ambaye
ni Mwenyekiti mwenza wa Taasisi ya Bill & Melinda Gates.



Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Bi. Margaret Chan
na Bw. Antony Lake wa UNICEF.



Akiwa hapa Rais pia atakutana na wadau wa sekta ya biashara na uwekezaji wa
Canada na Tanzania kabla ya kurejea Dar es Salaam.







Mwisho



Imetolewa na;


Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,

Toronto-Canada

28 Mei, 2014

No comments:

Post a Comment