Wednesday, 28 May 2014

MREMBO ACHANWA NA VIWEMBE KWA WIVU,eti kisa wivu,ashonwa nyuzi 28 kichwani,kifuani....soma mkasa mzima hapa



MREMBO ACHANWA NA VIWEMBE KWA WIVU,eti kisa wivu,ashonwa nyuzi 28 kichwani,kifuani....soma mkasa mzima hapa



INASIKITISHA
sana! Stela Mbinga ambaye ni mke wa mtu, mkazi wa Tegeta - Kontena
jijini Dar amepata balaa kubwa baada ya kuchanwachanwa uso wake kwa
viwembe na jirani yake aliyefahamika kwa jina la Zakia Mohamed.




Stella Mbinga akiwa na majeraha ya viwembe.
Habari
kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, Zakia na Stella kwa muda mrefu
wamekuwa wakiishi maisha ya uhasama na kuringishiana hali iliyojenga
chuki miongoni mwao.“Hawa huwa wanashindana kimaisha. Huyu akifanya
hivi, mwingine anafanya vile. Cha kushangaza huwa wanatishiana hadi
mambo ya vyakula, kwamba nani anakula vizuri zaidi ya mwenzake.
“Sasa
juzi Stella alikuwa amekaa kibarazani wanazungumza na shoga yake, Zakia
alipita akawakuta wanacheka, hata alipokuwa chumbani wakaendelea na
vicheko vyao, akahisi wanamsema na kumcheka yeye, alipotoka akamvaa
Stella, kumbe alikuwa na kiwembe, akaanza kumchana bila huruma,” alisema
mmoja wa majirani wa wanawake hao.
Wasamaria
wema walimpeleka Stella Kituo cha Polisi Tegeta ambapo ilifunguliwa
kesi nambari TGT/RB/1969/2014 - Kujeruhi kisha kukimbizwa katika
Hospitali ya Mwananyamala ambako alishonwa nyuzi 19 usoni na nane
kifuani.
Stella akiuguza majeraha.
Akizungumza
kwa tabu nyumbani kwake, Stella alisema: “Amenionea tu, hapa sijisikii
vizuri. Nahisi kizunguzungu na giza kila ninaposimama, pia siwezi kula
vizuri chakula kwani kila ninapotafuna, kichwa kinaniuma sana.”


No comments:

Post a Comment